Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ana
mambo mengi ya kufanya kwa sasa, lakini siyo ripoti ya mtangulizi wake,
Nape Nnauye,
Uteuzi wa Nape ulitenguliwa akiwa anatarajia kukabidhi ripoti ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudaiwa kuvamia kituo cha Clouds
Media.
Waziri Mwakyembe amesema hawezi kutoka na kauli za papara na matamko ya
haraka haraka ambayo yanaweza kuleta matatizo siku za mbele.
Alisema ripoti ya Nape dhidi ya Makonda siyo kipaumbele kwake bali yapo
mambo mengi ya muhimu ya kufanya badala ya kuhangaika na jambo hilo
ambalo halijakamilika kisheria. “Nimekuwa naulizwa sana na waandishi
wakati naapishwa. Kwanza hiyo ripoti yenyewe sijaiona, lakini hata
nikiiona siwezi kuipeleka kwani haijakamilika, maana imehoji upande
mmoja,” amesema Mwakyembe.
Mwakyembe amesema akiwa kama mwanasheria kwa mujibu wa ibara ya 13 ibara
ndogo ya sita (a) na sheria ya jumla anaheshimu sana kanuni hivyo kitu
chochote lazima kiheshimu katiba na haki kwani mtu hawezi kuwa hakimu
katika suala lake mwenyewe.
Akizungumzia kuhusu kuboresha wizara yake, amesema atahakikisha anafanya
kazi kwa karibu na watendaji wake ili kuifanya wizara hiyo kuwa na
maendeleo ya haraka.
Amesema kuna mambo mengi ambayo hatahaikisha anayafanya ikiwa ni pamoja
na kuhunganisha wasanii ili kuondokana na tofauti zao na badala yake
waunganishe nguvu ya kufanya kazi zao.
Pia Mwakyembe amesema atashughulikia usimamizi wa umaliziaji wa sera ya
sanaa na filamu ikiwa ni pamoja na kupambana na mahalamia wa wizi wa
kazi za wasanii.
No comments:
Post a Comment