Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam
leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa
vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa
kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa
msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote
waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa
kwa wiki nzima.
Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari;
magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za
Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi
kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.
Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu.
Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum
(Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza
habari zake hatutazichapisha.
Bodi inakipongeza Kituo cha Clouds kwa kumsimamisha kazi mtangazaji
aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda. Bodi pia
imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu
uendelee.
Theophil Makunga,
Mwenyekiti TEF
Imetolewa Leo,
Machi 30, 2017
No comments:
Post a Comment