Friday 31 March 2017

Rand ya Afrika Kusini yashuka kwa kasi

Fedha ya Afrika Kusini, rand, inaendelea kushuka thamani kwa kasi baada ya Rais Jacob Zuma kumtimua waziri wa fedha mwenye uzoefu mkubwa, Pravin Gordhan.
Zuma alitangaza uamuzi huo Alhamis hii kuwa anamuondoa Gordhan pamoja na mawaziri wengine. Wawekezaji walikuwa wameshaanza kuhofia kuwa Zuma angemtimua waziri huyo baada ya Jumatatu kumuamuru asitishe mikutano mingi na wawekezaji wa nje na kurudi nyumbani.
Hatua hiyo pia ilikuwa dhoruba kwa rand ambayo sasa imeshuka thamani yake kwa asilimia 8. Wachambuzi walionya mapema wiki hii kuwa kumuondoa Gordhan na mawaziri wengine kungekuwa na madhara.
Amekuwa waziri wa fedha kwa kipindi kirefu kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 na kurudi tena December 2015. Zuma amteua Malusi Gigaba aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kushika nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment