Friday 24 March 2017

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amekanusha taarifa ya Kinana Kuongea na Waandishi wa Habari

  Image result for humphrey polepole
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amekanusha taarifa zilizoenea leo asubuhi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Comrade Abdulrahman Kinana atakutana na waandishi wa habari.
Taarifa hiyo ilidai kuwa leo Ijumaa saa nne, Kinana ataongea na waandishi wa habari katika ofisi za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.


“Napenda kukanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba Katibu Mkuu wa CCM Komrade Kinana atakuwa na Mkutano na waandishi leo. Asante,” ameandika Polepole kwenye Twitter.

No comments:

Post a Comment