Uzinduzi wa uhamaji mtandao wa simu bila kubadilisha namba
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame M.Mbarawa akiongea na wadau mbalimbali wa Masuala ya Mawasiliano
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa Jumatano
hii amezindua rasmi huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda
mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani inayojulikana
kitaalamu kama (Mobile Number Portability(MNP). Chini ni picha zaidi za
uzinduzi huo.
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame M.Mbarawa akiwa
katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wanaotoa huduma za
mawasiliano za simu za mkononi,Watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya
sheria wa Vodacom Tanzania,Nina Pendael Eshun,Mara baada ya Waziri huyo
kuzindua rasmi huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda
mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani inayojulikana
kitaalamu zaidi kama (Mobile Number Portability (MNP).Hafla hiyo
ilifanyika makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo
jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment