Ukame mbaya unaokumba Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini humo.
Siku ya Jumanne Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, alitangaza ukame huo kuwa janga la kitaifa.
Umoja wa Mataifa una kadiria watu milioni tano nchini Somalia, wanahitaji msaada wa dharura na kuongeza kuwa taifa hilo ni moja kati ya mataifa manne, yaliyo katika hatari ya kukumbwa na janga la njaa.
Mataifa mengine ni Nigeria, Sudan kusini na Yemen.
Karibu watu 260,000 walifariki kutokana na baa njaa iliyokumba Somalia kuanzia mwaka 2010 na 2012.
Watu wengine 220,000 walifariki kutokana na njaa ya mwaka 1992.
Pia njaa imetangazwa katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, ambayo ndiyo ya kwanza kutangazwa tangu ile ya Somalia ya mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment