Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema
endapo atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini
atajiuzulu nafasi yake kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu yake katika
nchi huru.
Waziri Nape Nnauye
Nape ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia na kulaani kitendo
kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,
cha kuvamia chombo cha habari cha Clauds, akiwa na askari wenye silaha
na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.
Waziri huyo amesema amezoea kuona matukio kama hayo yanatokea kwenye
nchi ambazo zimepinduliwa kwa bunduki lakini kwa nchi yetu si jambo jema
kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki mkononi.
"Tumezoea kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa
kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa jambo hili
tunataka kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini
amefanya jambo hili". Alisema Nape
Kufuatia tukio hilo Waziri Nape ameunda tume yenye wajumbe takribani
watano itakayoenda kumhoji Makonda na kutoa mrejesho wa kazi hiyo ndani
ya masaa 24 ikiwa imeeleza sababu maalum kutokea kwa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment