Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Dk Dalali Kafumu na
makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, kwa pamoja wamejiuzulu nafasi zao.
Viongozi hao wameeleza sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ni serikali
kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo wakaeleza kuwa
hawaoni sababu za kuendelea na majukumu hayo.
Wamekabidhi barua za kujiuzulu kwenye ofisi ya spika wa bunge jana.
No comments:
Post a Comment