Na Masanja Mabula -Pemba ..
Madaktari
kisiwani Pemba wametakiwa kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani juu ya
vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea siku hadi siku dhidi ya
wanawake watoto, ili wasipoteze muelekeo wa kupata fursa za kiuchumi
nchini.
Hayo
yalielezwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Pemba Khadija Khamis Rajab katika hospitali ya Wete,
ikiwa ni shamra shamra ya siku ya wanawake duniani.
Alisema
kuwa, iwapo wanawake na watoto watadhalilishwa ndoto zao hukatika na
kutofikia malengo aliyoyakusudia yanayoweza kumpatia fursa za ajira
katika kujiimarisha kiuchumi.
Afisa
huyo alisema kuwa, zipo kesi ambazo madaraktari wanahusika na
udhalilishaji kwa wanawake na watoto na kuwataka kuwa mstari wa mbele
katika kutoa ushahidi wa vipimo mahakamani pindi unapotokea udhalilishaj
huo.
Hata
hivyo alipongeza juhudi zinazofanywa na baadhi ya madaktari akiwemo
Sauda Kassim wa hospitali ya Chake Chake kutokana na kuwa mstari wa
mbele kutetea na kutoa ushahidi wa kutosha mahakamani na kumuhudumia
muathirika ipasavyo.
Kwa
upande wake daktari msaidizi katika hospitali hiyo, Kulthum Bakar Juma,
ameeleza kuwa kutokana na udhalilishaji wanaofanyiwa mahakamani pamoja
kuona watuhumiwa wanaachiwa huru bila kutiwa hatiani linawarudisha nyuma
madaktari katika kutoa ushahidi mahakamani.
Nae
Daktari Asya Omar Abrahman kutoka kitengo cha Benki ya Damu katika
hospitali hiyo amesema, wamekuwa wakipoteza muelekeo wanapotakiwa kutoa
ushahidi mahakamani, kwani mwisho wa siku mtuhumiwa anaonekana mitaani
na kurudia tena udhalilishaji bila ya kuogopa.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8, ikiwa ujumbe wa mwaka huu unasema ‘imarisha fursa za ajira kumuwezesha mwanamke kiuchumi’.
No comments:
Post a Comment