Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru
akitoa mada leo kwenye semina ya siku moja kwa wakurugenzi, wakuu wa
idara na wakuu wa vitengo kuhusu majukumu na wajibu wao katika
kutekeleza shughuli zao za kila siku.
Baadhi
ya wakurugenzi, wakuu wa idara na wakuu wa vitengo katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) wakifuatilia mada kwenye semina ya siku moja
iliyofanyika Leo katika hospitali hiyo.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto,
Dk. Magreth Mhando akiwaeleza viongozi hao vipaumbele ambavyo wanapaswa
kuvizingatia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Mkuu wa Idara ya Maslahi na Mahusiano Kazini wa hospitali hiyo, Noorani Valli akisisitiza jambo kwenye semina hiyo leo.
Baadhi ya wakuu wa idara, wakurugenzi na wakuu wa vitengo wakifuatilia kwa makini semina hiyo leo.
Bwana Buma akiuliza swali kwenye semina hiyo leo.
Mkuu wa Idara ya Manunuzi, Bwana Pindani Nyalile akitoa mada kwenye semina hiyo leo.
Na John Stephen, Dar es Salaam 17.03. 2017
Wakurugenzi,
wakuu wa idara na wakuu wa vitengo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), wametakiwa kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi
wanaowasimamia na kujali maslai yao ili kuleta mageuzi makubwa ya kutoa
huduma bora kwa wagonjwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru ameyasema hayo leo
wakati wa semina ya siku moja ya kuwakumbusha viongozi hao majukumu yao
ya kila siku.
“Viongozi
mnatakiwa kuwa wabunifu, msilalamike kuhusu changamoto zinazowakabili,
jambo mnalopaswa kufanya ni kutatua changamoto kwa manufaa ya hospitali
ya Muhimbili,” amesema Profesa Museru.
Profesa
Museru amewaagiza wakuu wa idara, wakuu wa vitengo na wakurugenzi
kuhakikisha MNH inatoa huduma bora kwa kuzingatia wanashiriki kikamilifu
katika utekelezaji wa kujenga miundombinu ya kisasa ya kutoa tiba kwa
wagonjwa.
Naye
Mwakilishi Kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Magreth Mhando amesema MNH inatakiwa kuzingatia vipaumbele
vya taifa katika Sekta ya Afya ambavyo ni kuboresha huduma ya afya kwa
mama na mtoto ili kupunguza vifo katika kundi hilo.
Dk
Mhando ametaja vipaumbele vingine ni kuweka nguvu kwenye bima za afya
ili kuongeza mapato, kuweka mikakati ya kutoa mafunzo kwa ajili ya
kuimarisha utoaji huduma kwa wateja na kupungunza idadi ya wagonjwa
wanaokwenda kutibiwa nje kama serikali inavyosisitiza.
Katika
hatua nyingine, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Makwaia Makani amewataka
wakuu wa idara na vitengo kusimamia kwa makini utendaji kazi wa
wafanyakazi wanaowasimamia kwa lengo la kuimarisha utoaji bora wa huduma
kwa wagonjwa.
“Mkuu
wa idara anapaswa kutambua idadi ya wafanyakazi anaowasimamia na kujua
kama wanaripoti kazini kila siku. Mfanyakazi ambaye hayupo kazini kwa
zaidi ya miezi miwili bila ruhusa, ni mfanyakazi hewa,” amesema Makani.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
No comments:
Post a Comment