Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo
lake mara baada ya Mbunge huyo kutoa msaada wa Baiskeli 120 zenye
thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 22 kwa ajili kutumika jimboni humo
katika shughuli mbalimbali za chama. Makabidhiano hayo yalifanyika
katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Misungwi ambapo makatibu wote Wa matawi
walikabidhiwa baiskeli hizo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu akizungumza na Wanachama wa CCM wa
Jimbo la Misungwi mara baada ya Katibu huyo kukabidhiwa Baiskeli 120
zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22 na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga
(wanne kulia mstari wa mbele). Baiskeli hizo walikabidhiwa makatibu wote
wa matawi wa CCM jimboni humo ili ziweze kurahisisha usafiri katika
kazi mbalimbali za chama jimboni humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (kulia) akimkabidhi Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya
shilingi Milioni 22, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa
Mwanza, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kuwakabidhi makatibu wa matawi wa
CCM Jimbo la Misungwi ili ziweze kutumika kwa ajili ya Shughuli za chama
jimboni humo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya
Chama hicho, mjini Misungwi.
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kushoto)
akiwakabidhi Baiskeli baadhi ya makatibu wa matawi wa CCM wa Jimbo la
Misungwi, mara baada ya Katibu Huyo kukabidhiwa Baiskeli 120 zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22, na Waziri wa Mambo Ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga (kulia).
Baiskeli hizo ambazo zitatumika katika shughuli za kichama jimboni humo
zilikabidhiwa katika ofisi za chama hicho, mjini Misungwi leo.
Tigo Yafungua Duka jipya wilayani Handeni
Mkuu wa willaya ya Handeni Mhe. Halima Rajab Msangi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles na wafanyakazi wa Tigo wa duka
la Handeni mara baada ya uzinduzi uliofanyika mapema ya wiki wilayani
Handeni mkoani Tanga.
Rais Magufuli achangia shilingi milioni 10 upanuzi wa kanisa Chato
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Mchango wa Shilingi Milioni 10
kwa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili
kuchagia upanuzi wa kanisa hilo.
Fedha hizo zimekabidhiwa na Kaimu
Mnikulu Bw. Ngusa Samike katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya
pili ya Pasaka, iliyofanyika kanisani hapo leo tarehe 03 April, 2016.
Kabla ya misa hiyo ya pili Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na Waziri Mkuu
Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga,
walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia
shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao
unaendelea.
Katika Misa hiyo Paroko wa Parokia
ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia
kuadhimisha miaka 50 ya tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na
kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao
unachangiwa na waumini wenyewe.
Padre Mulinganisa amemshukuru Rais
Magufuli kwa mchango huo, na amemuahidi kuwa utatumika vizuri ili
uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na michango ya waumini wengine.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
03 April, 2016
No comments:
Post a Comment