Mchezaji
wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu akizungumza na wanahabari baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es
Salaam jana usiku kwa mwaliko wa siku tano wa Kampuni ya Vizimbuzi ya
StarTimes.
Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu alipokuwa akiwasili Uwanja wa Ndege.
Hapa
Kanu akihojiwa na wanahabari. Kushoto na kulia ni Mabaunsa waliokuwa
wakimlinda baada ya kufika Uwanja wa Ndege kabla ya kuelekea Hoteli ya
Serena.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Be. Lanfang Liao (kulia),
akimuelekeza jambo mchezaji huyo wakati wakielekea kupanda gari kuelekea
Hoteli ya Serena. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa
StarTimes Tanzania, William Masy.
KAMPUNI
inayojihusisha na utoaji wa huduma za matangazo ya luninga kwa njia ya
dijitali, StarTimes Tanzania imepokea ugeni mzito wa aliyekuwa mchezaji
nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Bw.
Nwankwo Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa kampuni hiyo kwa bara la
Afrika ambamo imo kwenye takribani nchi zaidi ya 10.
Akizungumza mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jana usiku, mchezaji Nwankwo Kanu alisema kuwa anajisikia furaha kubwa kuwasili Tanzania salama kujumuika na kmapuni ya StarTimes katika Shughuli mbalimbali kwa ndani ya kipindi cha siku tano atakazokuwepo.
‘’StarTimes ni kampuni kubwa
barani Afrika na imeleta mapinduzi makubwa katika upande wa matangazo
ya luninga kwa dijitali kwani imeweza kutoa huduma Zake kwa ubora mkubwa
na gharama nafuu ambazo kila mtu anaweza kuzimudu.’’
Kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo mchezaji Kanu amebainisha kuwa kampuni ya StarTimes imepiga hatua kubwa hasa kwa upande wa kupata na kuonyesha michezo ya ligi ya soka kubwa barani Ulaya kama vile za Bundesliga na Serie A za Ujerumani na Italia.

“Mimi kama balozi wa StarTimes barani Afrika nitajitahidi kawa kadiri ya uwezo wangu kuwa kiungo muhimu katika kuhakikisha ninaiwakilisha vema kwa wateja wake, hususani katika shughuli mbalimbali kama vile soka kama mjuavyo ni mchezo unaopendwa na watu wengi duniani na hata miongoni mwa waafrika wenyewe.” Aliongezea Kanu.
“Hivyo basi kwa muda wote
nitakaokuwepo nchini Tanzania nitashirikiana na StarTimes kwa ukaribu
katika shughuli za kikampuni na pia za kijamii kama vile za kielimu na
afya. Kama mjuavyo katika mahala popote unapofanyia shughuli zako Ni
muhimu sana kuijali jamii inayokuzunguka kwani yenyewe ndiyo sababu
kubwa ya wewe kuwepo.” Alihitimisha
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini, Bw. Lanfang Liao amesema kuwa, “Uwepo wa Kanu Tanzania ni fursa ya kipekee na pia ni moja ya jitihada kubwa za kampuni yake katika kuimarisha na kuhudumia wateja wao hususani kwa vipindi Vya michezo na burudani na ninaamini uwepo wake utaleta chachu kwetu sisi na wateja kwa ujumla.”
“Nwankwo Kanu alikuwa ni mchezaji wa kimataifa si tu aliiwakilisha nchi yake ya Nigeria kimatifa katika michuano mbalimbali lakini pia alifungua milango kwa vipaji vya Afrika barani Ulaya. Hivyo basi tunaamini bado ni maarufu na ana heshima kubwa miongoni mwa watanzania na wapenda soka barani Afrika. Kwa Yeye kuwa balozi wetu ninaamini tutafaidika kwa namna gani tuboreshe huduma Zetu ili kuiteka mioyo ya watanzania na waafrika kiujumla.” Alimalizia Bw. Liao

WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA YA KIKAZI IFAKARA, MOROGORO
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiongea na wananchi katika hospitali ya Rufaa ya St. Francis pamoja na
wajawazito wanaosubiri kujifungua na ambao wapo chini ya uangalizi wa
madaktari.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
amefanya ziara ya siku 1 mjini Ifakara kufuatilia utendaji wa shughuli
mbalimbali za Afya Wilayani Kilombero, Morogoro.
Katika
ziara hiyo, Mhe Ummy ambae alieambatana na Balozi wa Uswisi nchini
Tanzania, Mhe Florence Tonguely-Mattli alifungua kozi ya miezi mitatu ya
kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kina mama wajawazito hususani
katika eneo la upasuaji na utoaji wa dawa za usingizi.
Mafunzo
hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya (TTCIH)
chini ya Mradi wa “Upatikanaji wa Uzazi Salama Tanzania” yanawahusisha
Washiriki 70 kutoka mikoa ya Morogoro, Njombe na Mbeya.
Mhe
Ummy pia alikagua shughuli mbalimbali za taasisi za afya ikiwemo
kutembelea Taasisi ya Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute),
Hospitali Teule ya Rufaa ya St. Francis, Chuo cha Uunguzi cha Edgar
Malanta na Chuo Kikuu cha Tiba cha St. Francis.
Mhe
Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya
Kimataifa ya Afya (TTCIH) Prof. Pemba, Balozi wa Uswisi nchini Mhe
Florence Tonguely-Mattli.
Picha ya pamoja.
Mhe.
Ummy Mwalimu akiongea na washiriki wakati wa kufungua mafunzo ya miezi
mitatu ya kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kinamama wajawazito mjini
katika taasisi ya TTCIF, Ifakara.
No comments:
Post a Comment