Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide
Na Tabu Mullah
Msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide, Amefunguka kuwa katika wimbo wake mpya wa Ndindindi, hajampiga kijembe aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash kama wengi Wanavyodhani.
Jide na aliyekuwa mumewe, Gardner
Akizungumza na Fofam Blog , Jide alisema Wimbo huo Ulitungwa na watu Wake Tofauti na Yeye kuukamilisha hivyo kwa kuwa umebeba ujumbe mzito ni Rahisi ,tu kuhisi amemuimba mtu fulani kumbe yeye aliimba kwa ajili ya Mashabiki wake wote.
“Sijampiga kijembe huyo wanayemsema (Gardner). Mimi nimetumia utunzi Wangu kuwakilisha yale yanayotokea katika jamii mbalimbali sasa kama mtu Anaona umemgusa fulani atakuwa amejiongeza tu lakini mimi sikumaanisha mtu Mmoja bali ujumbe kwa mashabiki wangu wote,” alisema Jide.
Kwenye wimbo huo kuna sehemu Jide kaimba; “Niliwezaje kutoa vyote ili hali Wewe ulininyima vyote” ambapo iliaminika amemzungumzia Gardner.
No comments:
Post a Comment