Na Kalonga Kasati
KAMPUNI ya Total E&P Uganda imesisitiza kwamba bomba la mafuta Mazito kutoka Uganda, litajengwa kupitia ardhi ya Tanzania kwenda Bandari Ya Tanga, licha ya kuwepo kwa mazungumzo ya kushawishi lipite katika Ardhi ya Kenya kwenda Bandari ya Lamu, ambayo Haijajengwa.
Gazeti
la Kenya la Daily Nation liliweka taarifa hiyo jana katika mtandao Wake, ikimnukuu Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Adewale Fayemi Akisema njia
hiyo ni nafuu kwao.
“Msimamo
wa kampuni yetu umebakia kuwa bomba litakwenda Bandari ya Tanga,
naelewa kuna mambo yanaendelea kujadiliwa lakini msimamo wetu Umebaki
pale pale,” amekaririwa Fayemi na gazeti la Daily Nation.
Fayemi
amekaririwa akisema kabla ya kufikia uamuzi wa kupeleka bomba Hilo
kwenda Bandari ya Tanga, walifanya tathimini na kuangalia fursa zote.
Katibu
Mkuu wa Nishati wa Kenya, Joseph Njoroge, alipohojiwa Amekaririwa
akisema kama nchi yake ikikosa fursa ya kupitisha bomba Hilo katika
ardhi yake, Kenya itajenga bomba lingine bila kujali kama itapata Ushirikiano na Uganda au la.
Bomba
hilo kupita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga, kuna
unafuu mkubwa na utekelezaji wake utakuwa na ufanisi kutokana na
kutokuwepo tishio la ulinzi na usalama wa miundombinu kama ilivyo
Kenya.
Mbali
na unafuu na kutokuwa na tishio la usalama,Tanzania ndiyo yenye uzoefu
wa muda mrefu na wa hivi karibuni wa ujenzi, uendeshaji, ulinzi na Uelimishaji jamii katika miradi ya Bomba la mafuta.
Uzoefu
huo unatajwa kuwa ni wa ujenzi, uendeshaji na uhudumiaji wa Bomba la
Mafuta la Tanzania na Zambia (Tazama) tangu mwaka 1968, likitoka Dar es
Salaam mpaka Ndola Zambia. Bomba hilo lenye kipenyo cha Nchi 8 mpaka 12
na urefu wa kilometa 1,710; kati ya hizo kilometa 860 zipo kwenye ardhi
ya Tanzania na limekuwa likipitisha mafuta tani milioni 1.1 kwa mwaka.
Tanzania
pia ina sifa ya uzoefu wa ujenzi, uendeshaji na uhudumiaji wa Bomba la
gesi kutoka Songo Songo mpaka Dar es Salaam, lenye kipenyo Cha nchi 12
na urefu wa kilometa 25 kutoka kisiwa cha Songo Songo Mpaka
Somangafungu.
Pia
kuna bomba lingine la urefu wa kilometa 207 na kipenyo cha nchi 16,
kutoka Somangafungu mpaka Ubungo Dar es Salaam, mbali na bomba kubwa la
gesi kutoka Mtwara mpaka Kinyerezi Dar es Salaam lenye zaidi Ya kilometa
490.
Lipo
pia bomba la gesi linalotoka Mnazi Bay kwenda Mtwara, urefu wa kilometa
27 na kipenyo cha nchi 8, ambalo limeanza kutumika tangu 2006.
Akizungumza
hivi karibuni katika mahojiano na Shirika la Utangazaji (TBC),
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Dk James
Mataragio, alisema bomba hilo likipita Tanzania kwenda Tanga, kampuni Hiyo ya Total itapata nafuu ya Dola za Marekani milioni 500, sawa na
zaidi ya Sh trilioni moja za Tanzania.
Aliwataka
Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kushawishi na kuvutia Mradi huo,
kwa kuwa una faida za ziada zitakazoendana na mradi huo, ikiwemo
kuongezeka kwa wawekezaji na kujenga miundombinu ya Mawasiliano sambamba
na bomba hilo.
Bandari
ya Tanga iko tayari na ina mazingira wezeshi ya asili ikiwemo kina
kirefu kinachoruhusu meli kubwa kufunga gati bila usumbufu na kingo za
asili, wakati Kenya bandari inayokusudiwa ya Lamu haijajengwa.
Mpaka sasa,bandari
ya Tanga imeshakamilisha Tathimini ya Athari za Kimazingira (EIA) na
Upembuzi Yakinifu, wakati njia ya Tanga ya bomba Hilo imekwishaainishwa
na haitapitia katika hifadhi za taifa wala mapori ya Akiba.
Bandari
ya Tanga pia inayo fursa ya kutumika zaidi na mradi huo, kwa kuwa haina
msongamano wa shughuli za bandari na tayari Serikali ya Tanzania
kupitia Mamlaka ya Bandari (TPA), imeshatenga fedha za upanuzi Utakaohitajika na eneo.
Bandari
hiyo pia imeunganishwa kwa reli na barabara za lami, Zinazokwenda nchi
za jirani na hivyo iko tayari kuanza kutumika kwa ajili Ya kuingizia
mizigo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Bomba
hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,410 na litasafirisha mafuta Ghafi
mapipa 200,000 kwa siku kutoka Ziwa Albert nchini Uganda, hadi Bandari
ya Tanga na ujenzi wake unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa Moja
1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
No comments:
Post a Comment