Na Mwamvita Mtanda
Muigizaji wa Bongo Movies Shamsa Ford amesema kuwa anafurahishwa na maisha ya Uhusiano ‘usioyumba’ wa wanamuziki nyota wa Marekani, Jay Z na Beyonce.
Msanii huyo alisema kwamba Uhusiano wa kimapenzi wa Wasanii wa hapa nchini huwa si wa Dhati na kufanya kutodumu na hali hiyo inamfanya yeye kutojihusisha tena na uhusiano na Msanii mwenzake.
Kupitia akaunti yake ya Instagram,msanii huyo aliandika: ”uhusiano wa masta YaBey ndiyo pekee ninaouelewa miongoni mwa mastaa wengine,”.
Huku akiwa ameweka picha inayowaonyesha Beyonce na Jay Z aliendelea kusema kwamba kila siku anafurahia kuona maisha yao yanakuwa na furaha na kutaka nyota wengine waige Mfano huo.
”Hayo ndiyo mahusiano ninayoyakubali dunia nzima,” Shamsa aliongeza.
Alieleza kuwa mapenzi ya wasanii nyota wa hapa nchini si ya kutoka moyoni ila yanalenga kumfaidisha mmojawapo na anapofanikiwa huamua kuchana na mpenzi wake huyo.
No comments:
Post a Comment