Wednesday, 20 April 2016

Kabwe:Nipo Tayari kwa Uchunguzi Kama Sitahusika Nitalipwa Fidia


Kabwe: Ikigundulika nimeonewa nitalipwa fidia? nina uhakika ukweli utajulikana tu.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam ambaye Jana alisimamishwa kazi na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Wilson Kabwe ametaka Uchunguzi Ufanyike ili kubaini Ukweli kwamba amehusika na Ubadhirifu uliotajwa Jana na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Ama la.

Bwana Kabwe amesema kuwa, amekubaliana kusimamishwa kazi kwa kuwa Rais ni Bosi wake Na yupo Tayari kwa Uchunguzi Dhidi yake.

“Nimekwambia sina la kukwambia ila niseme tu sina shida na hilo, Uchunguzi ufanyike nina Uhakika Ukweli Utajulikana tu lakini kama ukijulikana ikibainika Nimeonewa kuna fidia Yoyote nitalipwa?” aliuliza


No comments:

Post a Comment