Kondakta wa Daladala, Hamim Seif (42) Mkazi wa Mwananyamala
Ujiji, Amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli kwa maneno.
Seif
alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana mchana na kusomewa Shtaka
hilo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kenneth Sekwao.
Mshtakiwa
huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa alisema kuwa Dhamana ya Mshtakiwa huyo iko wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini
wawili, kutoka Taasisi ya Serikali inayotambulika, ambaye atasaini Hati
ya Dhamana ya Sh2 milioni.
Licha ya Dhamana yake hiyo kuwa wazi, Mshtakiwa huyo alishindwa kukamilisha Masharti Hayo kwani baada ya
kusomewa mashtaka alipoulizwa kama alikuwa na Wadhamini alishindwa
kuwapata.
Akimsomea Shtaka linalomkabili, Wakili Sekwao alisema
kuwa Mshtakiwa huyo Alitenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya
Soweto, Makumbusho Wilayani Kinondoni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (a)
na kifungu cha 35 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.
Wakili Sekwao
alisema akiwa katika baa hiyo, mshtakiwa alitishia kumuua Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa maneno kwa njia ya
kujitoa mhanga.
“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli,
mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alisema
Wakili Sekwao akimnukuu mshtakiwa Huyo.
Hata hivyo, Wakili
Sekwao alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Akaomba Tarehe
nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.
No comments:
Post a Comment