Meya Ilala amekunjua Makucha Yake kwa Mhandisi wa Barabara
Na Kalonga Kasati
kutumbua majipu ni wimbo
unaopendwa na watanzania wengi, naimani watanzania Bado hawajalisahau
jipu lililo tumbuliwa jana na Rais Dkt John Pombe Magufuli wakati wa Uzinduzi wa daraja la Nyerere, ambapo ame msimamisha kazi Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala Wilson Kabwe.
Kutumbua majipu hakuchagui dini, rangi
wala kabila, au itikadi yeyote ile hivi ndivyo anavyo Uthibitishia umma
wa watanzania wengi Mstahiki Meya wa Ilala Charles Kuyeko baada ya Kuwatumbua watumishi watatu wa manispaa hiyo kwa usimamizi mbovu wa
miradi ya Barabara za wilaya hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo
Mstahiki Meya Kuyeko amesema wilaya yake imejipanga kusimamia miradi ya
maendeleo katika wilaya hiyo na kuwanufaisha wanachi Wote, hivyo
kutokana na kikao kilichofanywa na madiwani mwishoni wa wiki wameadhimia Kumsimamisha kazi Mhandisi mkuu Japhari Mwigane na watumishi wengine
ambao ni Siajari Mahili na Daniel Kiligiti.
Meya amesema watumishi hao wamekuwa
wakilalamikiwa kwa muda mrefu na madiwani wa Wilaya hiyo lakini wamekuwa
hawayafanyii kazi malalamiko hayo jambo ambalo limemplelekea meya
kuchukua hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi kutokana na usimamizi Mbovu wa
barabara, akiitolea mfano wa barabara ya Moshi Bar ambayo imeleta
athari kwa Wakazi wanaopita kwenye barabara hiyo.
Katika hatua nyingine Mstahiki Meya
Kuyeko ameeleza kuwa Manispaa yake imetenga bilioni 85 kusimamia miradi
ya maendeleo tofauti na bajeti za miaka iliyo pita hivyo anaimani
kutokana na bajeti hiyo itaweza kutatua suala la miundombinu, huduma za
Afya, suala la Elimu kwa kuongeza vyumba vya madarasa na madawati ambapo
wameishaanza kujenga Madarasa kuanzia matano mpaka nane kwa shule zenye
upungufu.
No comments:
Post a Comment