Wednesday, 20 April 2016

Gari aina ya Hiace imezama Katika Bahari ya Hindi ene la Kivukoni

0eb582f5-55e1-4ca1-a35f-9a839ed6f11e

Alfajiri  ya leo gari aina ya Hiace lililokuwa katika foleni ya kuingia katika kivuko Upande wa Posta kuelekea Kigamboni lilizama katika Bahari eneo la Kivukoni.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanaeleza chanzo cha gari hiyo kuingia na kuzama baharini kimetokana na kile kinachodaiwa kufeli kwa breki wakati dereva wa gari hiyo akikata kona kuelekea upande wa mbele ambapo gari zenye uharaka zinapewa nafasi kukaa mbele pindi kivuko kitakapofika ziwe za kwanza kuingia katika kivuko hicho.

Mashuhuda wanasema gari hilo lilipewa kipaumbele kwani inasemekana lilikuwa limebeba Waombolezaji waliokuwa wakienda msibani upande wa Kigamboni.

 cfbece29-fb5f-4a49-81ee-8080f6c9682f

Taarifa zaidi zinasema wakati dereva wa gari hilo akitafuta namna ya kuegesha (kupaki) gari Hilo ndipo gari hiyo ilipofeli breki na kuzama Baharini.

Ajali hiyo imesababisha Dereva wa gari hilo ambaye jina lake bado halifahamika kupoteza Maisha huku juhudi za uokoaji zikiendelea

No comments:

Post a Comment