Mwakilishi Maalum wa Umoja wa
Afrika (AU) katika mgogoro wa Libya, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete leo amekutana na Naibu Waziri wa
Mambo ya nje wa Italy Dk. Mario Giro, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu
ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo maalum.
Akizungumza na waandishi wa
habari baada ya mazungumzo, Msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa,
Suleyman Mwenda alisema, Dk. Kikwete amekuwa na mahusiano ya kirafiki ya
muda mrefu na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro,
hivyo Naibu Waziri huyo amefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kumjulia
hali kama rafiki yake wa muda mrefu.
“Pamoja na kuja kumsalimia kama
rafiki wa siku nyingi, lakini lengo hasa la Naibu waziri huyo ni kutaka
maelezo juu ya suala la Libya’ alisema Mwenda na kuongeza “Kama
mnavyofahamu kuwa Dk. Kikwete ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika (AU) kuwa
mwakilishi katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa Libya”.
Alisema, Italy inalipa umuhimu wa
kipekee suala la Libya kutokana na kwamba nchi hiyo ni jirani hivyo
ina maslahi mapana na ya karibu juu ya suala la amani ya Libya, Dk. Giro
ameiwakilisha nchi yake katika kujua hatua ya usuluhishi na hatma ya
mgogoro wa Libya.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri
huyo aliambatana na Balozi wa Italy hapa nchini, Luigi Scotto pamoja na
Dk. Raffaele De Lutio, Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Italy.
Shurika La Posta Lazindua HudumaMpyaYa PostaMlangoni Jijini Dar es salaam
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta
Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus
Kapinga, moja ya kifurushi kwa ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa
uzinduzi wa huduma hiyo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
(kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika
la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, moja ya kifurushi kwa
ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, huku
akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora (kushoto) na Mwakilishi wa
Umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU), Naibu Katibu Mkuu, Kola Aduloju
(mwenye miwani kulia).
Juu na Chini: Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa
Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akimkabidhi moja ya
kifurushi hicho, mfanyakazi wa Posta kwa ajili ya kukipeleka nyumbani
kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Kola Aduloju, akitoa hutuba yake katika uzinduzi wa huduma
hiyo.
Meneja Msaidizi wa Biashara ya Barua, Jason Kalile akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
(kushoto), akibonyeza kitufe cha kompyuta kwa ajili ya kuzindua rasmi
huduma hiyo, huku akishuhudiwa na Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu
wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga (wapili
kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Mawasiliano), Maria Sasabo (katikati).
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
(kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika
la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, moja ya kifurushi kwa
ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu
na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus
Kapinga, moja ya kifurushi kwa ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa
uzinduzi wa huduma hiyo, huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora
(kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU), Naibu
Katibu Mkuu, Kola Aduloju (mwenye miwani kulia).
TFF Kuwachukulia Hatua Kali,Viongozi Na Watumishi Wake
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa zilizosambaa katika mitandao
kuanzia jana zikiwahusisha viongozi wa timu moja ya daraja la kwanza na
baadhi ya watumishi wa TFF.
Pamoja na kwamba taarifa hizo
zilizosambazwa hazihusiani na kesi ya kupanga matokeo iliyoamuliwa siku
ya tarehe 03/04/2016, TFF inachunguza kubaini uhalisia (authenticity) wa
taarifa hizo na itachukua hatua kali sana kwa watumishi wa shirikisho
na viongozi wa timu husika watakaobainika kushiriki vitendo vilivyo
kinyume na maadili ya mpira wa miguu.
TFF imekwishaweka bayana nia ya
kupambana na yeyote atakayehusika katika upangaji matokeo na uhalifu
mwingine unaoharibu ustaarabu wa mpira kwa njia yoyote ile.
Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linatoa onyo kwa baadhi ya viongozi, watumishi wa TFF na
wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla wanaotumia majina ya viongozi wa juu
wa TFF katika kufanikisha mipango yao kwa manufaa binafsi.
TFF inawaomba wapenda mpira wa miguu kuwa watulivu na waangalifu wakati suala hili linashughulikiwa.
Aidha, kuhusu hukumu ya Kamati ya
Nidhamu ya TFF ni muhimu ikaeleweka wazi kwamba zipo taratibu za kukata
rufaa kwa mujibu wa kanuni ili upande usioridhika na maamuzi
yanayotolewa uweze kuhoji maamuzi husika.
Ni vema tukaacha kamati huru
zifanye kazi zake kwa mujibu wa taratibu. Kutoa hukumu mtaani au kwenye
vyombo vya habari kunaweza kuwanyima haki wanaostahili na kutengeneza
kichaka cha kujificha watenda maovu.
No comments:
Post a Comment