Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli amekataa daraja la Kigamboni lisiitwe 'Daraja la Magufuli' na badala yake ameshauri lipewe Jina la muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akiongea wakati wa kuzindua daraja hilo leo, Rais Magufuli amesema kuwa Awali aliletewa
mapendekezo na waziri mwenye dhamana akimtaka aridhie Daraja hilo
lipewe jina lake, lakini kwakuwa wazo la ujenzi huo lilianza tangu
wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, alikataa na kushauri jina la Nyerere litumike .
“Nilikataa
lisiitwe kwa jina langu kwa sababu wazo la ujenzi wa daraja hili
lilianza mwaka 1979 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.
"Wazo
hilo halikufanikiwa kutokana na ukosefu wa pesa wakati huo. Mwalimu
Nyerere ni kiongozi aliyejenga misingi imara katika taifa letu.
"Alikuwa
ni kiongozi asiyebagua mtu kwa misingi ya dini, chama au kabila.
Alifanikiwa kutuunganisha watanzania wote bila kujali itikadi zetu.
"Leo
hii, daraja hili limekamilika, ni daraja ambalo halitambagua mtu kwa Sababu wa CCM watapita hapa, wa Chadema watapita hapa na bahati nzuri Mstahiki Meya wa jiji hili ambaye ni Chadema naye yuko hapa na amepita
katika daraja hili.
"Ndugu
zangu sistahili sifa zozote, najua nimefanikisha ujenzi huu nikiwa
waziri wa ujenzi, lakini wakati huo nilikuwa natimiza wajibu wangu kama Mtumishi wa umma, hivyo nashauri hili daraja liitwe daraja la Nyerere
ili Tuweze kumuenzi mwasisi wa taifa hili” alisema Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha
wanalitunza daraja hilo katika kujenga uchumi wa taifa.
No comments:
Post a Comment