Monday, 29 August 2016
Mwanasheria Mkuu wa Serikali avionya vyama vya siasa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aonya vyama vya siasa kutumia maneno yanayovunja amani na usalama wa nchi.
Masaju ambaye amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo, ametolea mfano Oparesheni UKUTA iliyotangazwa kufanywa na CHADEMA na kusema kuwa ina maneno ya kijeshi yanayotumiwa kwenye shughuli za kihalifu.
Lema apandishwa mahakamani Arusha
Dar es Salaam. Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika kesi mbili tofauti.
Kesi ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa
uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu
tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”
Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano Septemba Mosi kinyume cha sheria.
Mgeja ataka Jaji Mutungi, Dk. Mwakyembe wajiuzulu

Dk. Harrison Mwakyembe
Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Hamisi Mgeja amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, wajiuzulu kwa kile alichodai kuwa wameshindwa kumshauri Rais John Magufuli katika masuala yanayohusu Katiba na Sheria.
Mgeja pia amepinga kauli ya Rais Magufuli kutaka kupiga mnada majengo ya serikali baada ya kuhamia Dodoma.
Akizungumza Dar es Salaam , Mgeja alisema watu hao wameshindwa kuzitumikia vema nyadhifa zao kumshauri Rais katika masuala ya Katiba na Sheria na kusababisha mvutano mkubwa unaochagizwa na kuvunjwa kwa haki za katiba za vyama vya siasa kufanya shughuli zao.
Asamoah Gyan arudi Uingereza

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Sunderland anafanyiwa ukaguzi wa matibabu na klabu hiyo ya daraja la kwanza.
Gyan aliifungia mabao 30 Sunderland alipoichezea timu hiyo kwa misimu miwili,kutoka mwaka 2010 kabla ya kuelekea Al-Ain ya Umoja wa Milki za kiarabu UAE.
Alijiunga na Shanghai 2015 wakati huo na alikuwa miongoni mwa mchezaji wanaolipwa zaidi duniani.
Mkwasa ampumzisha Dida Taifa Stars, kipa wa JKT Ruvu apata ulaji

Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi ambaye amefiwa na baba yake mzazi katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016.
Kipao alikuwa nyota wa mchezo katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na mechi ikaisha kwa sare ya bila bao huku yeye akionyesha umahiri mkubwa wa kuokoa michomo ya washambuliaji na viungo wa Simba.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni:
Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC
Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - Genk ya Ubelgiji
Vyombo vya usimamizi wa Sheria vyatakiwa kutoa adhabu mbadala kwa wahanga wa dawa za kulevya nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole
nchini Dkt. Augustine Mrema (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar
es Salaam na kuwaeleza umuhimu vyombo vya usimamizi wa sheria nchini
kutoa adhabu mbadala ya kifungo cha nje kwa wahanga wa matumizi ya dawa
za kulevya nchini ikiwa ni sehemu ya barua yake kwa Rais John Magufuli.
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole
nchini Dkt. Augustine Mrema (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao kuwaeleza umuhimu
vyombo vya usimamizi wa sheria nchini kutoa adhabu mbadala ya kifungo
cha nje kwa wahanga wa matumizi ya dawa za kulevya nchini ikiwa ni
sehemu ya barua yake kwa Rais John Magufuli, kulia ni Dkt. Bingwa wa
Magonjwa ya Akili toka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Cassian
Nyandindi na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bw. Vincent
Tiganya.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini Dkt. Augustine Mrema
(hayupo pichani) wakati alipokutana na waandishi hao leo jijini Dar es
Salaam kuwaeleza umuhimu vyombo vya usimamizi wa sheria nchini kutoa
adhabu mbadala ya kifungo cha nje kwa wahanga wa matumizi ya dawa za
kulevya nchini ikiwa ni sehemu ya barua yake kwa Rais John Magufuli.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo.
Na Eliphace Marwa -MAELEZO -Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Bodi ya Taifa ya
Misamaha kwa Wafungwa (Parole) Dkt. Augustine Mrema amevitaka vyombo vya
usimamizi wa sheria nchini kutoa adhabu mbadala ya kifungo cha nje kwa
wahanga wa matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Hatua hiyo inaeelezwa itawezesha
kuwapatia huduma bora za matibabu ambazo ni ngumu kuzipata pindi wawapo
mahabusu au wakitumikia kifungo katika magereza.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Jijini Dar es Salaam, Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Tanzania Labour Party (TLP) alisema katika siku za hivi karibuni
kumezuga tabia kwa baadhi ya askari polisi kuwageuza mtaji wahanga wa
madawa ya kulevya.
“Natoa wito kwa Jeshi la Polisi
kuacha mara moja tabia ya kuwabambikia kesi wahanga hawa na badala yake
washughulike na wakubwa wa wauza madawa hayo ambao wapo katika jamii na
wanafahamika na hata baadhi ya Polisi” alisema Dkt. Mrema
Aidha Mrema alisema idadi ya
watumiaji wa madawa ya kulevya imekuwa ikiongezeka kila kukicha nchini
hatua inayoisababisha Serikali kuwa mzigo mkubwa katika kuwahudumia
ikilinganisha na mahitaji yaliyopo.
Tamasha la Uhondo wa Zantel lakonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
:Meneja Habari na Uhusiano wa
kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia) akitoa
maelezo kwa baadhi ya wakazi wa Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la
Dares Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu huduma mpya zitolewazo na kampuni
hiyo ikiwa ni moja ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya
katika kuboresha bidhaa zake na kutoa huduma bora kwa wateja. Ilikuwa
ni katika tamasha lililopewa jina la Uhondo wa Zantel lililodhaminiwa na
kampuni hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
anayetesa na wimbo wake maarufu wa ‘Unanitega Shemeji’, Selemani Jabil
‘MsagaSumu’ akifanya vitu vyake wakati wa tamasha la ‘Uhondowa Zantel’
lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Zantel.
Meneja Habari na Uhusiano wa
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia) akitoa
zawadi kwa mmoja wa washindi wa maswali ya papo kwa papo wakati wa
tamasha la ‘Uhondo wa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam. Tamasha hilo lililodhaminiwa na Zantel kama
sehemu ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika
kuboresha bidhaa zake na kutoa huduma bora kwa wateja.
Serikali yaahidi kutoa ushirikiano kwa TECC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi.
Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa
Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw.
Sosthenes Sambua na Meneja wa Ofisi wa TECC, Bi. Mwasiti Mkembe (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi.
Jenista Mhagama (kushoto) akimkabidhi kitabu cha Mpango Kazi wa miaka
miwili cha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo, Bi. Beng’i Issa wakati
wa uzinduzi rasmi wa TECC mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi.
Beng’i pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi.
Jenista Mhagama (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bi. Beng’i Issa
(wa pili kulia); mjumbe wa bodi hiyo, Dkt. Hassan Mshinda (katikati) na
Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua (kushoto) wakati wa
uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Bi. Issa pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) wakati Dkt. Mshinda pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
|
Sehemu ya wadau mbalimbali
walioshiriki uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani
Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Habari/Picha Na Ally Daud.
|
Serikali imeahidi kutoa
ushirikiano kuhakikisha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania
(TECC) inastawi na kufaidisha wananchi kwa kupitia miradi yake
mbalimbali kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.
Akizungumza hayo katika uzinduzi
rasmi wa TECC Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa
watendelea kuwa pamoja na Taasisi hiyo ili kufikia malengo ya watanzania
kiuchumi.
“Kwa niaba ya serikali natambua
mchango wa wajasiriamali hivyo tupo pamoja na TECC kwa kila jambo
watalofanya kwa ajili ya kusapoti uchumi wa nchi kupitia ujasiriamali
katika kuelekea uchumi wa viwanda.” Alisema Mhe. Jenista
Mbali na hayo Mhe. Jenista amesema
kuwa malengo ya TECC ni kuimarisha ubunifu na ushindani wa biashara
ndogo na za kati za Tanzania kwa kuwavuta wajasiriamali waliopo ndani ya
sekta isiyo rasmi, wahitimu wa vyuo na wengine wenye kutaka kuanzisha
biashara zinazoongeza thamani kwa mazao na kutengeneza bidhaa nchini.
Aidha Mhe. Jenista amesema kuwa
Biashara zikianzishwa nyingi na nyingi zikijipanua kiushandi ndivyo na
serikali itapata mapato zaidi kupitia kodi hivyo uzalishaji uongezeke
zaidi na zaidi kwa maendeleo ya nchi.
Chama cha Waajiri (ATE) chazindua tuzo za Waajiri Bora 2016 jijini Dar leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha
Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari jijini kuhusu tuzo za Mwajiri Bora 2016
zinazotarajiwa kutolewa mwezi Disemba mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika
katika ofisi za ATE,jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko,
Mawasiliano na Mradi, Joyce Nangai.
Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na
Mradi, wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Joyce Nangai (kushoto)
akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka.
Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakirekodi wakati Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Aggrey Mlimuka
akizungumza nao kuhusu tuzo za mwaka huu za Waajiri Bora zinazotarajiwa
kutolewa baadae mwaka huu.
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
leo kimezindua Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2016 kutambua Waajiri wenye
misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili
kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji
kibiashara.
Akizungumza kwenye Mkutano na
Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka
alisema kwamba lengo kuu la Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka ni kutambua
wanachama wenye sera nzuri za usimamizi wa rasilimali watu.
Alisema kuwa kwa miaka kadhaa tuzo
hiyo imesaidia kuhamasisha wanachama kujikita katika kushughulikia
masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama msingi muhimu
katika kumwezesha mwajiri kuwa na wafanyakazi wenye kukikidhi ushindani,
wanaojituma na wenye furaha.
Aliongeza kuwa tuzo hiyo ilifuata
mbinu za kisayansi na kitaalamu ili kuangalia umuhimu wa Rasilimali
Watu katika makampuni ya kibiashara kuanzia makampuni makubwa kwa
madogo na yale ya kati ili kuinua ujuzi na kuwa na wafanyakazi wenye
kufanaya kazi kwa kujituma kama njia ya kutoa motisha kwa wafanyakazi
ambao ndio msingi wa rasilimali watu.
Aliongeza kuwa EYA lilikuwa tukio
muhimu linalofanywa na ATE kila mwisho wa mwaka tangu mwaka 2005.
Alisema kuwa tuzo hiyo imekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa
biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa
wa kati kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya kufanya biashara
nchini.
Aliongeza kuwa tukio hilo la
kutafuta mshindi limegawanyika katika makundi makuu mawili ambapo
litaanza na kufanya utafiti kwa kutumia Mshauri Mwelekezi na hatua ya
pili itakuwa ni hafla ya kutoa tuzo yenyewe kwa washindi ambalo
litafanyika mwezi Desemba 2016.
“Tukio hili limegawanyika katika
makundi mawili, ambapo hatua ya kwanza ni kufanya utafiti na hatua ya
pili ni hafla ya kutoa tuzo kwa washindi,” alisema.
Tahadhari ya kiafya yatolewa kupatwa kwa jua
Tukio la kupatwa kwa jua
Tahadhari imetolewa kwa wakazi wa mikoa ambayo itashuhudia
kupatwa kwa jua kuwa kutazama jua moja kwa moja bila kutumia kifaa
chochote kunadaiwa kuwa na madhara kwa mtazamaji kutokana na mionzi ya
jua hilo.
Kupatwa kwa jua kunatarajiwa kutokea katika mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini ya Njombe wilaya ya Wang'ing’ombe katika kijiji cha Litundu,
Mbeya wilayani Mbarali katika kijiji cha Mpungarelini na mkoani Katavi
ambako kupatwa kwa jua kutaonekana vizuri kwa zaidi ya asilimia 97.WCB Wasafi kufungua ofisi mpya Kijitonyama

Akiongea katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Jumatatu hii, mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam, amesema wanafungua ofisi mpya ili kuipa nafasi ofisi ya zamani ya kufanya shughuli zake bila kuingiliana na shughuli zingine.
“Tunafungua ofisi nyingine ya WCB Kijitonyama,” alisema Sallam.“Hii itakuwa kwa ajili ya viongozi, halafu ile nyingine nitaendelea na kazi nyingine,”
WCB kwa sasa ni moja kati ya label za muziki ambazo zinafanya vizuri kutokana na wasanii wake wengi kufanya vizuri.
Shamsa Ford kufunga ndoa Ijumaa hii

Msanii wa filamu Shamsa Ford anatarajia kufunga ndoa Ijumaa hii na mfanyabiashara wa nguo aitwae ‘Chidi Mapenzi’.
Muigizaji huyo ameiambia FOFAMMEDIA kuwa ndoa hiyo itafanyika nyumbani kwa wazazi wake Sinza Africana jijini Dar es Salaam.
“Kweli bhana Ijumaa hii Mungu akipenda nafunga ndoa,” alisema Shamsa Ford.
Miezi mitatu iliyopita mfanyabiashara huyo alikiri kuwa kwenye mahusiano na malkia huyo wa filamu na kuweka wazi mpango ya ndoa.
Waziri Nape Nnauye awataka Watanzania kuwapa Moyo Wanamichezo nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akimkabidhi cheti Mwanariadha
Alphonce Simbu baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya tano katika
Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akimkabidhi
King’amuzi cha Kampuni ya DSTV Mwanariadha Alphonce Simbu baada ya
kuibuka mshindi wa nafasi ya tano katika Mashindano ya Olimpiki
yaliyomalizika hivi karibuni mjini Rio, Brazil.

Rais wa Shirikisho la
Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akiongea na baadhi ya Viongozi,
wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo (hawapo pichani) walioshiriki
katika Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni
mjini Rio, Brazil.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Olimpiki (TOC) Bw. Filbert Bayi akiongea na baadhi ya Viongozi,
wageni waalikwa pamoja na Wanamichezo (hawapo pichani) walioshiriki
katika Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni
mjini Rio, Brazil.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape
Nnauye amewataka Watanzania kujifunza kuwatia moyo Wanamichezo
wanaposhiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Wito huo ameutoa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa Hafla
ya kuwapongeza na kupokea bendera ya Taifa toka kwa Wanamichezo ambao
walishiriki katika Mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni
mjini Rio, nchini Brazil.
Pius Msekwa amewaasa watanzania kuacha kufuata mkumbo wa kisiasa

Msekwa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu mwenendo wa siasa za hapa nchini na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Alieleza kuwa watu wengi wana hulka ya kufuata mkumbo kwenye mambo fulani bila ya kuchunguza na kufahamu ukweli wake kabla ya kushabikia.
Hatimaye Drake na Rihanna mambo hadharani


Radio 5 FM na Magic FM zafungiwa kwa muda usiojulikana
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya Redio kurusha matangazo yao.
Waziri Nape ametangaza uamuzi huo hivi punde katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuzitaja redio hizo kuwa ni Radio 5 FM ya Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaam.
Misri imepitisha sheria kali dhidi ya Ukeketaji

Picha inayopinga ukeketaji
Hukumu ya miaka kumi na mitano inaweza kutumika pale ambapo kitendo hicho cha ukeketaji kitasababisha ulemavu. Ukeketaji umekuwa ni suala lisilokubalika kisheria nchini misri tangu mwaka 2008 lakini vitendo hivyo vya ukeketaji vimekuwa vikienea kila uchao nchini humo.
Jose Mourinho ampiga mkwara Rashford

Rashford alitokea katika benchi akichukua nafasi ya Juan Mata katika dakika za mwisho za pambano hilo la kusisimua lililopigwa Uwanja wa KCOM jijini Hull na dakika chache baadaye akaifungia Man United bao la ushindi.
Rashford bado hajaanza mechi yoyote chini ya Mourinho licha ya kutamba katika msimu uliopita akiwa na Kocha aliyetimuliwa, Louis van Gaal kiasi cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kilichoshiriki michuano ya Euro nchini Ufaransa.
Sunday, 28 August 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)