Saturday, 30 September 2017

Man U yazidi kupasua mawimbi Chelsea wakishikwa shati na Man City

Timu ya Manchester United imezidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kutafuta ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi mnono wa jumla ya magoli 4-0 dhidi ya Vibonde Crystal Palace mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Traford.
Magoli ya Man United yakifungwa na Fellaini aliyefunga mawili dakika ya 35 na 49,Juan Mata dk 3 na Lukaku 86.
Kwa Matokeo hayo Man United wanabaki kwenye nafasi yao ya pili wakiwa na alama 19 sawa na Man City wakiwa wanatofautiana magoli ya kushinda na kufungwa Vijana wa Mourinho wamefunga magoli 21 na kufungwa mawili huku Guardiola akiwa ameshinda magoli 22 na kufungwa mawili.
MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 7, Jones 7, Smalling 6.5, Young 7; Matic 6, Fellaini 8; Mata 7.5 (Herrera 76 mins, 6), Mkhitaryan 5.5 (Lingard 66, 6), Rashford 7 (Martial 71, 7); Lukaku 6 
Subs not used: Bailly, Blind, Romero, Darmian
Goals: Mata 3mins; Fellaini  35, 49; Lukaku 86 
CRYSTAL PALACE (4-3-3): Hennessey 6; Ward 5.5, Sakho 6, Delaney 5.5, van Aanholt 6; Townsend 6, Milivojevic 6, Puncheon 5.5 (Riedewald 69, 5.5); Cabaye 6.5, Sako 6.5 (Ladapo 74), Schlupp 5.5 (McArthur 69, 6) 
Subs not used: Speroni, Lee, Mutch, Kelly
Referee: Mike Dean 6
Attendance: 75,118
Kevin De Bruyne sent the travelling fans into raptures with his brilliant finish to put City ahead in the second half
Katika uwanja wa Darajani wenyeji Chelsea wamepoteza mechi yao baada ya kufungwa goli 1-0 na Manchester City huku Chelesea wakipata pigo kutokana mshambuliaji wao Moratta kupata majeraha.
Goli la ushindi la Man City limefungwa na Kevin De Bruyne kipindi cha pili kwa shuti kali na kumshinda mlinda mlango dakika ya 67 Courtois
The Belgian scored with a well placed shot from the edge of the box which left Thibaut Courtois with no chance

Mkutano wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi

1
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam.
2 3
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam.
5
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe. Dkt. John Magufuli akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Rodrick Mpogolo kabla ya kufungua mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)   jijini Dar es Salaam.
6
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam.
7
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam.
8
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam.
9 11
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es Salaam.
12
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiendelea na Kikao jijini Dar es Salaam.
13
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiendelea na Kikao jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Habari Picha

PICHA 1
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo hufanyika kila mwisho wa mwezi. IGP amewahimiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya pamoja ili kuendelea kuboresha afya za maofisa na askari.
PICHA 2.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo hufanyika kila mwisho wa mwezi. IGP amewahimiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya pamoja ili kuendelea kuboresha afya za maofisa na askari.

Halmashauri ya Kinondoni yasaini mikataba ya shilingi bilioni 49.


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumjuri amesaini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara mbele ya mstahiki meya Benjamini Sitta yenye thamani ya shilingi bilioni 49.
Katika miradi hiyo itakayohusisha barabara ya Makanya, kisiwani, tandale, simu2000 ,  Ubungo external, kilingowima ni muendelezo wa awamu ya pili na tatu ya miradi ya uendelezaji wa jiji hilo DMDP, 
Kwa upande wake Mstahiki meya Benjamini Sitta ameyataka makampuni hayo jenzi (Estim na China Civil Engenearing Corp)  kuzijenga barabara hizo kama walivyokubaliana kwa kuwa barabara hizo ni muhimu mpaka kwa manispaa ya za jirani ikiwemo ya Ilala.
Hata hivyo amewataka wananchi wa maeneo husika kuhakikisha wanaitunza miundombinu ya barabara hizo mara baada ya kukamilika.

Tanzania yapata msaada wa sh bilioni 29.4 kutoka China

Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong.
Katibu huyo amesema 22.4bilioni  zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera.
“Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema   James
Ameeleza kwamba  kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho.
“Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” amesema  James
Katibu Mkuu huyo amesema China, itatoa 6.7bilioni kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
“Katika makubaliano yetu ya msaada wa kuendeleza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000, China itatoa msaada wa kiufundi na vifaa vya kisasa vya michezo na utaalamu katika usimamizi na ukarabati wa uwanja” Amefafanua James

Amesema  kiasi kingine cha shilingi 300milioni zitatumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuanzishwa kwa aina mpya ya utalii ujulikanao kama utalii wa kijiolojia “Geopark Project” katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, mkoani Arusha.

Alisema lengo la utafiti huo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na maajabu mbalimbali ya kitalii yaliyopo nchini ambayo hayajatumika kikamilifu kuvutia watalii watakaoongeza pato la Taifa
“Tanzania ina kila sababu ya kujifunza kutoka katika Hifadhi ya Kimataifa ya Jiolojia ya Jiaozuo ya Yuntaishan ya China, iliyoanzishwa mwaka 2000 ambayo inaongeza asilimia 37.2 ya watalii kila mwaka na huchangia asilimia 12 ya pato la Taifa la nchi hiyo”
Tangu miaka ya 1960 mpaka sasa nchi hiyo imeendelea kuisaidia  Serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo upanuzi wa Chuo cha Polisi Moshi, Ujenzi wa Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong, amesema ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Veta huko Ngara mkoani Kagera utaanza haraka kama ilivyopangwa.
Kuhusu masuala  ya utalii wa kijiolojia katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, amesema Tanzania ina bahati ya kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini haijavutia idadi kubwa ya watalii kutoka China kuja kuvitembelea.
“Zaidi ya watalii milioni moja kutoka China wanatembelea nchi mbalimbali dunia lakini kati ya hao, Tanzania inapokea watalii 20,000 tu kila mwaka kutoka China, lakini kwa kuanzisha mradi huu, watalii wengi kutoka China watavutiwa kuja nchini kufurahia utalii wa miamba, mandhari nzuri, urithi wa dunia, na kutembelea hifadhi za Taifa” ameongeza Haodong
Akizungumzia masuala ya uchumi, Balozi huyo amesema  hivi sasa China imekuwa mwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania kwa kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani 1.77bilioni  na kukuza ajira nchini.

Waziri wa afya nchini Marekani, Tom Price ameachia ngazi

Waziri wa afya nchini Marekani, Tom Price amejiuzulu baada ya kukodi ndege binasfi ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za kiserikali.
Waziri Price aliomba radhi kwa kufanya safari akitumia ndege za kukodi mara 26 tangu mwezi May kwa gharama za dola za kimarekani 400,000 zikiwa ni fedha za walipa kodi nchini humo.
Nchini Marekani maafisa wa serikali isipokuwa wale wanaoshughulikia masuala ya usalama wanatakiwa kutumia ndege za abiria katika safari za kikazi. Habari zinasema mawaziri wengine watatu katika utawala wa Trump wanachunguzwa kwa kutumia ndege binafsi za kukodi kwa shughuli za serikali.
Taarifa ya Ikulu imesema Rais Trump ameridhia kujiuzulu kwa Price na tarifa hiyo kuainisha kwamba Don J Wright atakaimu nafasi hiyo kwa sasa Wright ni Naibu Waziri wa Afya katika serikali hiyo.

Wachezaji 5 waliomfukuzisha kazi Kocha Ancelotti


Masaa kadhaa baada ya Carlo Ancelotti kupoteza ajira yake katika klabu bingwa ya Ujerumani – FC Bayern Munich kutokana mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha – Rais wa klabu hiyo Uli Hoeness ametaja moja ya sababu kuu zilizosababisha uongozi wa Bayern kuamua kuivunja ndoa yao na Ancelotti.
Uli Hoeness anasema kulikuwa na wachezaji wakubwa watano ambao walishakuwa hawana imani na kocha na walianza kumpinga.
“Kulikuwa na wachezaji watano ambao walikuwa wanampinga na hilo likawa jamho gumu kwenye utendaji wa kazi,” aliiambia Funke Sport.
“Kama kocha huwezi kuwa na wachezaji wakubwa kwenye kikosi chako ambao wanakupinga. Nimejifunza hili maisha yangu yote na msemo usemao; Adui aliyepo kitandani kwako ndio hatari zaidi.’ Kutokana na jambo hilo ilitubidi kuchukua maamuzi magumu dhidi ya Mr. Ancelotti.”
Carlo Ancelotti akiwa na Bayern Munich ana rekodi ya kuiongoza katika mechi 60, wameshinda 42, sare 9 na wamepoteza mechi 9. Timu yake ilifunga magoli 156, na pia waliruhusu magoli 50 kutinga kwenye nyavu zao. Ameshinda Bundesliga mara moja na DFL Supercup mara 2.

Roketi kuanza kusafirisha watu



Itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Hivi karibuni watu wataweza kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine kutumia roketi, safari ambayo itachukua dakika chache tu, kulingana na mjasiriamali Elon Musk.
Musk aliahidi haya katika kongamano moja nchini Australia.
Inasemekana kuwa itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Musk amesema pia kuwa mwaka wa 2024, ataanza kuwasafirisha watu hadi Mars. Kampuni yake ya SpaceX itaanza kujenga meli za kipekee zitakazofanikisha haya, mwaka ujao.
Kwa sasa kampuni yake inatengeneza ain amoja tu ya roketi; aina ya BFR ambayo inaweza kufanya kazi tofauti tofauti ikiwemo kupeleka watu kwenye mwezi na Mars.
"Safari ambazo watu wengi wanaona kuwa ndefu zinaweza kukamilika kwa chini ya nusu-saa," aliambia umati wa watu mjini Adelaide.
"Baadhi ya wateja wetu wanataka kuona BFR ikiruka mara kadhaa kabla yaya kuwa na imani nayo," Musk alisema.
"Kwa hivyo tunachotaka kufanya ni kujenga roketi kadhaa aina ya Falcon 9 na Dragon, ili wateja wawe na urahisi, na ikiwa wanataka kutumia roketi za kale, bado tuna kadhaa."
Musk, alianza mipango ya kufanikisha safari za Mars mwaka wa 2016, na amerejea na habari zaidi.
Musk amevutia watu wengi sana ambao wamependezwa na miradi yake. Na ingawa ahadi zake mara nyingi zimechukua muda mrefu kutekeleza, baadhi imetimia.

Friday, 29 September 2017

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPT 30 2017




Raia Mwema lafungia kwa miezi mitatu

Image result for raia mwema
Serikali imesitisha uchapishaji na usambazaji wa gazeti la kila wiki la RAIA MWEMA kwa muda wa siku 90 (miezi mitatu) kuanzia leo. Agizo hili pia linahusu toleo la mtandaoni. Adhabu hii inatokana na toleo na. 529 la tarehe 27 Septemba–3 Oktoba, 2017 lililochapisha habari ya uchambuzi inayosomeka “URAIS UTAMSHINDA JOHN MAGUFULI.”
Serikali inasisitiza uchambuzi huu ni maoni yao ya haki (fair comment), hata hivyo, kwa bahati mbaya, na nia ovu, makala hiyo ilisheheni nukuu za kutunga na zisizo za kweli zikimsingizia Rais John Pombe Magufuli. Gazeti hili pia limepata kuonywa huko nyuma kwa makosa mbalimbali.  
Nukuu za uongo, kutungwa na zenye nia mbaya zikidai Rais alipata kusema: “Suruali za zamani msizitupe, mtazihitaji baadae,” na “Watakaobaki  Dar es Salaam baada ya mwezi wa saba watakuwa wanaume kwelikweli.
Walipotakiwa kuthibitisha wapi iwe ndani au nje ya nchi Rais alipata kutoa kauli hizo, wahariri wa RAIA MWEMA waliomba muda, wakapewa. Wakarejea na kuthibitisha kuwa hawana ushahidi huo, wakakiri kosa na kuomba radhi.
Bado Serikali inaamini kwamba Watanzania tukiufanyia mzaha upotoshaji wa taarifa na uchochezi katika zama hizi za TEHAMA amani na utulivu tulivyojivunia kwa miaka mingi vitapotea na kukaribisha maafa kama ilivyotokea kwingineko duniani.
Serikali, katika uamuzi huu, uliochukuliwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Waziri wa Habari katika kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari Na. 12, 2016, imetoa adhabu ndogo tofauti na ukubwa wa kosa kwa kuwa wahariri wa gazeti hili hawakufanya tashtiti, wamekiri kosa.
Hata hivyo katika suala hili tunajifunza tena mambo kadhaa kuhusu changamoto za kiwango cha weledi wa uandishi wa habari nchini kiasi inatulazimu kutoa ufafanuzi wa kina kwa faida ya umma na tasnia yenyewe; kwamba uandishi ni taaluma adhimu na yenye haki na wajibu vinavyopaswa kufuatwa na si kufanyiwa dhihaka. 
Mintaarafu, mmoja wa wanasiasa waasisi wa Taifa la Marekani wanaotambulika kuwa waumini wakubwa wa uhuru wa habari, Thomas Jefferson, pamoja na kupigania sana uhuru huo, katika barua kwenda kwa rafiki yake, James Madison, wakati wa mjadala wa katiba mpya nchini humo alisisitiza wajibu wa vyombo vya habari hasa katika “….kutodhalilisha heshima ya mtu au kuharibu amani na utulivu….”
Kwa upande wake, John Stuart Mills, Muingereza anayetajwa kuwa “Baba wa Haki ya Kujieleza” ambaye katika kitabu chake mashuhuri cha “On Liberty” alitetea sana uhuru wa habari, naye alitambua umuhimu wa kutekeleza haki kwa kulinda haki za wengine alipoandika:
The only freedom which deserves the name is that of pursuing our own good in our own way, so long as we do not attempt to deprive others of theirs, or impede their efforts to obtain it.”
Aidha, Mahatma Gandhi, Baba wa Taifa la India na mpigania uhuru na haki asiyetiliwa shaka, naye aliamini katika uhuru wa habari lakini alionya vyombo vya habari lazima vitimize wajibu wao wa kutoandika uongo na uzushi aliposema:
I venture to suggest that rights that do not directly from duty well performed are not worth having…. The superficiality, the one-sidedness, the inaccuracy and often even dishonesty that have crept into modern journalism, continuously mislead honest men who want to see nothing but justice done.”
Mitazamo hii ya kifalsafa ya magalacha hawa mashuhuri duniani, imeenziwa na kutiliwa nguvu katika mikataba na sheria mbalimbali za kimataifa za haki za binadamu ambazo nchi yetu pia imeiridhia. Kifungu cha 19(3) cha Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kisiasa na Kiraia ambao Tanzania imeuridhia tangu mwaka 1976, kinasisitiza wajibu huu kikisema:
“3. The exercise of the rights provided for in paragraph 2 of this article carries with it special duties and responsibilities. It may therefore be subject to certain restrictions, but these shall only be such as are provided by law and are necessary:  (a) For respect of the rights or reputations of others;  (b) For the protection of national security or of public order (ordre public), or of public health or morals. 

Mitandao ya Kijamii yalaumiwa kwa Kudhalilisha wanawake na Viongozi

Pix 01
Mjumbe wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Saum Rashid akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa, katikati ni Bi. Angelina Mutahiwa na kulia ni Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa Sekretarieti hiyo.
Pix 04
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mjumbe wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Angelina Mutahiwa (aliyekaa katikati) wakati wakitoa karipio juu udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa.
Pix 02
Mjumbe wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Angelina Mutahiwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa, kushoto ni Bi. Saum Rashid na kulia Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa Sekretarieti hiyo.
Pix 03
Mjumbe wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Angelina Mutahiwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa, kushoto ni Bi. Saum Rashid na kulia Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa Sekretarieti hiyo.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

Na Thobias Robert- MAELEZO
29-09-2017
Taasisi isiyo ya kiserikali inayoundwa na Jumuiya za Wanawake wa Vyama vyote vya siasa (Ulingo) imelaani vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii vinavyofanywa na baadhi ya watu dhidi ya viongozi wanawake wana siasa pamoja na serikali kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Saum Rashid alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwaaajili ya kulaani watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima viongozi wanawake.
“Matusi ambayo wanatupiwa na watu wasio na maadili ni matusi siyo kwa wahusika tu bali kwa wanawake wote, hivyo ikumbukwe kuwa hao wanaowalenga wanafamilia, watoto na marafiki na wanaongoza mamilioni ya watanzania,” alifafanua Bi. Saum.
Akizungumza bila kuwataja wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kudhalilisha viongozi, Bi.Saum alisema wanawake wanapodhalilishwa hasa na wanawake wenzao inawakatisha tamaa katika kutimiza majukumu yao hivyo akaomba mamlaka husika kusimamia Sheria ili mitandao isitumike vibaya.
Aidha Bi. Saum amesema kuwa anaamini viongozi wanawake ambao wamepewa heshima na dhamana ya kuongoza, wana uwezo mkubwa na wanastahili kuwa kwenye nafasi walizo nazo .
Taasisi hiyo ambayo inawashirikisha pia watu wenye ulemavu imelaani vikali vitendo vya udhalilishaji na kuwataka watanzania warejee kwenye misingi ya utu na kuthaminiana kama maadili ya kitanzania yanavyoelekeza hasa kwa watoto wa kike.
Kwa upande wake Angelina Mutahiwa ambaye pia ni Mjumbe wa taasisi ya Ulingo alisema kuwa, mwanamke ni mlezi mzuri wa maadili katika jamii hivyo kumdhalilisha ni kuvunja malezi na maadili katika jamii na kuchochea vitendo viovu dhidi yake ambavyo vitadumu kizazi hadi kizazi.
 “Wale wachache ambao wameonesha utovu wa nidhamu kwa kuendelea kumnyanyasa mwanamke watambue kwamba wao hawapo juu ya sheria na katiba ya nchi iko wazi hairuhusu mwanamke kudhalilishwa, kuonewa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili haikubaliki na hatutakubali,” alisistiza  Bi.Mutahiwa.

Serikali Yaipongeza Muhimbili kwa Kutoa Huduma Bora

0001A
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya (kulia) akitembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo ili kuona maeneo mbalimbali yaliokarabatiwa vikiwamo vyumba vya upasuaji na vyumba vya kulaza wagonjwa wa figo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.
0002
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Uzingizi leo pamoja na watumishi wengine wa hospitali hiyo
0003
Baadhi ya wafanyakazi wa idara hiyo pamoja na watumishi wengine mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya  leo.
0004
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya kuzungumza na wafanyakazi wa idara hiyo leo.
0005
Wafanyakazi wa Muhimbili wakiwamo wa Idara ya Usingizi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Museru.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili
Dar es salaam
Serikali imepongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) za kuboresha huduma  sanjari na kuwawezesha  watalaam kusoma ili wapate ujuzi zaidi na kutoa huduma bora na za kibingwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulusubisya wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo kupitia Idara ya Usingizi.
Dk. Mpoki amesema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na uongozi wa hospitali na kwamba hatua hiyo inaleta faraja kwa Watanzania kwani sasa wana uhakika wa kupata huduma bora .
“Naona mabadiliko makubwa hapa Muhimbili, mmeongeza vyumba vya upasuaji, Vyumba vya wagonjwa mahutuni (ICU) na pia mnaendelea kuboresha  huduma zingine kwakweli hatua hii ni ya kupongezwa na ninaomba muendelee kujituma kwani hospitali hii inategemewa kwa sababu  mna watalaam wengi waliobobea hapa,’’ amesema Dk. Mpoki.
Kuhusu kusomesha wataalam, Katibu Mkuu amesema hatua hiyo ni nzuri kwani watalaam hao watapata fursa ya kuwatawafundisha wengine ili nao wapate ujuzi .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema MNH inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalam katika Idara ya Usingizi na kwamba hospitali inaendelea kutatua changamoto hizo.
Dk. Mpoki ambaye ameambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dk. Doroth Gwajima pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwemo vyumba vya upasuaji, wodi ya wagonjwa mahututi na wodi ya watoto.

Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani

DSC_0817
Muakilishi wa Jimbo la Mpendae Said Mohd Dimwa wapili kushoto akifuatana na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
DSC_0827
Maandamano yalioongozwa na Bend ya Chipukizi yakielekea katika Ofisi ya Jumuia ya watu wenye maradhi yasioambukiza katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
DSC_0837
Vikundi mbalimbali vya mazoezi vikishajiisha suala zima la ufanyaji mazoezi ili kulinda afya na maradhi mbalimbali, katika siku ya maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
DSC_0852
Makamo mwenyekiti wa ZNCDA Ali Zubeir Juma akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
DSC_0890
Mgeni rasmi katika maadimisho ya siku ya Moyo Duniani Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Said Mohd Dimwa akitoa hotuba kuhusiana na kujikinga na maradhi mbalimbali yanayotokana na Ulaji,Unywaji wa Pombe na Uvutaji wa Tumbaku katika maadhimisho hayo yliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
DSC_0903
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kupimwa afya zao katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Habari Picha

1
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wapili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (katikati), mchoro wa ramani ya nyumba za Polisi za kisasa zitakazojengwa kufuatia za awali kuteketea kwa moto. Hatua ya ujenzi imeanza mara moja kufuatia Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, kutoa kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Hanspaul, Kamaljit Singh, na kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (DCP) Charles Mkumbo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Wakala ya Majengo Arusha Bw. Victor,.
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiagana na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alipomtembelea ofisini leo tayari kwa safari ya kurejea Dar es salaam, baada ya kuwapapole na  kukagua eneo la nyumba za Polisi zilizoteketea kwa moto.
Picha na Jeshi la Polisi.

Dkt. Mwakyembe Apiga Marufuku Matumizi ya Takwimu za Kampuni ya Geopoll

Pix 1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa na kulia ni Mjumbe kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Raynold Mfungahema
Pix 2
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
Pix 3
Mwakilishi kutoka kampuni ya IPSOS inayokusanya takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji Bw. Samuel Muthoka akiwasilisha taarifa ya namna kampuni hiyo inavyofanya kazi wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam.
Pix 4
Mwakilishi kutoka African Swahili  Televisheni akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam.
Pix 5
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa watatu kulia) katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
Na. Neema Mathas- MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku matumizi ya takwimu zinazotolewa na kampuni ya GeoPoll zinazohusu Kiwango cha wananchi kusikiliza na kutazama vituo vya Redio na Televisheni hapa nchini kwa kuwa takwimu hizo zina mapungufu makubwa.
Waziri Mwakyembe alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na makampuni ya ukusanyaji na usambazi wa takwimu kwa upande mmoja na watumiaji wa takwimu ambao ni vituo vya Redio na Televisheni kwa upande mwingine.
Katika kikao hicho cha pamoja, makampuni ya IPSOS Tanzania, Push Observer na GeoPoll walifafanya mawasilisho ya namna wanavyokusanya takwimu wakati Ofisi ya Taifa ya Takwimu yenyewe ilifanya wasilisho la kuonesha njia bora na sahihi za ukusanyaji na usambazaji takwimu. Hata hivyo kamapuni ya Geopoll haikuhudhuria kikao hicho.
“Nimeamua kuzuia utumiaji na usambazaji wa takwimu za kampuni ya GeoPoll hapa nchini baada ya kugundua tafiti za hii kampuni zina mapungufu makubwa na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau na wamiliki wa vituo mbalimbali vya radio na televisheni,” alieleza Waziri.
Kutokana na kupigwa marufuku matumizi ya takwimu za GeoPoll nchini, Waziri pia ameyataka makampuni yanayofanya uwakala wa kusambaza matangazo katika vituo vya Televisioni na Redio kusitisha kutumia takwimu za kampuni hiyo kama kigezo cha kutoa matangazo kwa vituo vya Televisheni na Redio.
Aidha Dkt. Mwakyembe alifafanua kuwa kama nchi haiwezi kwenda kwa utaratibu huu, kwani dunia ya leo ni ya biashara na ushindani ni mkubwa ambao unaendana na kujiuza na kujitangaza kwa chombo husika, hivyo alihoji “utajiuzaje kwenye soko kama watu wanaotakiwa kubeba matangazo yako wanatoa taarifa zinazosema kuwa wewe ni mdogo wakati ni mkubwa?.”
Dkt. Mwakyembe ameunda kamati ya watu watatu inayohusisha Idara ya Habari (MAELEZO), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo itafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wadau katika kikao hicho na na mwishoni mwa mwezi wa kumi iwasilishe mapendekezo ya namna bora ya ukusanyaji na usambazaji takwimu kwa mujibu wa sharia na taratibu.
Mmoja wa wachangiaji katika kikao Bi. Basilisa Biseko kutoka  vituo vya Radio na Televisheni alishauri Serikali iweke viwango vya namna ya kufanya utafiti wa takwimu ambavyo vitatumika na makampuni yote ya takwimu, lengo likiwa ni kuondoa udanganyifu na kutofautiana katika taarifa mbalimbali za idadi ya wasilikilizaji wa radio na watazamaji wa runinga.