Kikosi hicho kinachonolewa na kocha mkuu, Mzambia, George Lwandamina, kwa sasa kinashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara nyuma ya vinara Simba kwa tofauti ya pointi tano ambapo Simba inaongoza ikiwa nazo 54.
Ruvu inakutana na Yanga ikiwa inashika nafasi ya kumi, huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa mabao 2-1. Akizungumza na Championi Jumatano, Lwandamina alisema baada ya kupoteza dhidi ya Simba, sasa macho yao yote wanayaelekeza kwa Ruvu.
“Lazima tukubali tumepoteza mchezo kwa sababu katika soka kuna matokeo ya aina tatu, kushinda, kufungwa na sare, sisi tumepata moja kati ya hayo ambayo si mazuri kwetu.
“Kilichobaki sasa ni kuangalia tunafanya nini kwenye mchezo ujao ambao huo ni lazima tushinde, inatulazimu kusaka ushindi ili kurudi kwenye mbio za ubingwa,” amesema Lwandamina.
Naye Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire, amesema: “Vijana wangu wapo tayari kwa mchezo huo, kwa kuwa Yanga ilishauawa na Simba, sisi tunakwenda kuwazika tu, hawana nafasi ya kuchukua pointi kwetu.”
Wakati huohuo, Juma Abdul wa Yanga anatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na kupata majeraha kwenye mechi dhidi ya Simba na hadi jana alikuwa hajafanya mazoezi na wenzake.
No comments:
Post a Comment