Mbunge Tundu Lissu(CHADEMA) amekamatwa na Polisi asubuhi ya leo nyumbani
kwake Dodoma na kupelekwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi na sasa
anasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka masharti ya
dhamana.
Mbunge Tundu Lissu alikamatwa na jeshi la polisi asubuhi hii nyumbani
kwake na kupelekwa ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma.
==>Huu ni Ujumbe wa Tundu Lissu alioutumia mtandaoni
Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma.
Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya
kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS.
Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka
ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo
ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS.
Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya
serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi.
Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania:
Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za
binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu
yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii.
Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani
mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa
kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama???
Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.
Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu.
Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu.
Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za
watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza
hili nene. Msikubali kuyumbishwa.
Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu.
Nawatakieni kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take
me to, wherever I'll be incarcerated. This too shall pass. The race of
man shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende
Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences.
No comments:
Post a Comment