Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi
na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati)
akimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi katika mazungumzo na
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Japani (JICA), Bw. Toshio Nagase (kulia) katika hafla fupi ya kupokea
magari mawili (2) yaliyotolewa na JICA leo katika ukumbi wa JICA.
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa
JICA, Bw. Toshio Nagase (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya
Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba
(katikati) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari kwa Ofisi ya Rais
-Utumishi katika ukumbi wa JICA mapema leo. Wa kwanza kushoto ni Mshauri
wa Masuala ya Mahusiano kwa Umma wa JICA, Bw. Raymond Msoffe.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha
Ugavi na Ununuzi wa Ofisi ya Rais–Utumishi, Bw. Peter Mabale akihakiki
vibali vya mojawapo ya gari lililokabidhiwa kwa Ofisi ya Rais – Utumishi
kutoka JICA.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi
na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati)
akipokea funguo za magari kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-Utumishi Dr. Laurean Ndumbaro kutoka kwa Mwakilishi Mkazi
Mwandamizi wa JICA Bw. Toshio Nagase (kushoto) katika ofisi za JICA
mapema leo.
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Rais-
Utumishi na JICA mara baada ya hafla ya makabidhiano ya magari katika
ofisi za JICA jijini Dar es salaam.
Ofisi ya Rais-Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo imekabidhiwa magari mawili kutoka
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kwa matumizi ya
ofisi.
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa
JICA Bw. Toshio Nagase akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema
JICA imekabidhi magari hayo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati
ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na JICA.
JICA imetoa msaada wa magari kwa Ofisi ya Rais-Utumishi ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya ofisi hizo mbili.
Wakati wa hafla hiyo, Mwakilishi
wa Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Mick Kiliba alisema Tanzania imekuwa kati ya
nchi zinazonufaika na misaada kutoka nchini Japan.
“ Japan imekuwa ikiisaidia
Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo Elimu, Miundombinu, Afya, Maji
na Maendeleo ya rasilimaliwatu na leo ninafuraha kuona ushirikiano huu
unaendeleza urafiki wetu” Bw. Kiliba alifafanua.
Bw. Kiliba aliishukuru JICA na Serikali ya Japani kwa msaada wa magari hayo.
“Kwetu sisi ni msaada mkubwa
sana. Magari haya yataleta mabadiliko chanya kwa kuongeza uwajibikaji na
utoaji huduma bora kwa umma”
Bw.Kiliba aliahidi kuwa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI itahakikisha inayatunza na kuhakikisha yanafanikisha lengo
la Ofisi la kutoa huduma bora.
No comments:
Post a Comment