Saturday, 4 March 2017

Niger yatangaza hali ya hatari mpakani na Mal


Serikali ya Niger imetangaza hali ya hatari katika maeneo saba yanayopakana na Mali.
Tangazo hilo lililotolewa moja kwa moja kupitia runinga ya kitaifa, linasema hatua hiyo imechukuliwa katika harakati ya kujibu shambulizi hatari lililotekelezwa na wanamgambo waliyo na ufungamano na vugu vugu la umoja wa makundi ya kijihadi Afrika magharibi lililo na makao yake katika maeneo hayo ya mpakani.

Mamlaka ya Niger inawalaumuwanamgambo hao kwa kushambulia wanajeshi katika kambi ya wakimbizi.
Chini ya tangazo hilo la hali ya hatari, jeshi linaweza kufanya msako wa nyumba hadi nyumba muda wowote.

No comments:

Post a Comment