Marouane Fellaini (kushoto) akishangilia na Jesse Lingard (kulia) baada
ya wote kufunga katika ushindi wa Manchester United wa 3-1 dhidi ya
wenyeji Middlesbrough leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa
Riverside. Fellaini alifunga la kwanza dakika ya 30, Lingard la pili
dakika ya 62 na la tatu lilifungwa na Antonio Valencia dakika ya 90 na
ushei, wakati la kufutia machozi la Boro lilifungwa na Rudy Gestede
dakika ya 77.
No comments:
Post a Comment