Wednesday, 1 March 2017

Madaraja 8 mpakani mwa Tanzania na Malawi Yamevunjwa

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Ileje mkoani Songwe,imebaini na kuyavunja madaraja 8 yaliyojengwa kinyemela kwa ajili ya kuvushia magendo zikiwemo dawa za kulevya na wahamiaji haramu.
Kamati hiyo ya ulinzi na usalama chini ya mkuu wa wilaya ya Ileje,Joseph Mkude ameongoza Opesheni hiyo kwa kuyavunja madaraja hayo nane yaliyojengwa juu ya miti kwa ajili ya kuvusha magendo,dawa za kulevya na wahamiaji haramu.
Kufuatia operesheni hiyo,kaimu mkuu wa polisi wilayani humo,Ntwale Twale,amesema jeshi la polisi limekuwa likifanya doria pembezoni mwa mpaka huo,na kufanikiwa kuwakamata waharifu wa makosa mbalimbali,huku mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Haji Mnasi akisikitishwa na jinsi halmashauri inavyopoteza mapato kutokana na wafanyabiashara hao kutumia njia za panya kuvusha bidhaa.

Wananchi raia wa Malawi na Tanzania kwa upande wao licha ya kuipongeza kamati ya ulinzi na usalama kwa kubaini madaraja hayo na kuiomba kamati hiyo,iongeze nguvu ili kujenga mahusiano mema baini ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment