Azam FC wametupwa nje ya mashindano ya Caf Confederation Cup kufatia
kipigo cha magoli 3-0 ugenini dhidi ya Mbabane Swallows ya Swazland.
Mchezo wa kwanza ulichezwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam
Complex, Chamazi-Dar es Salaam, Azam walipata ushindi mwembamba wa goli
1-0.
Kichapo cha goli 3-0 kilichoiondoa Azam mashindanoni, kimekuja siku moja
baada ya mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC kuondoshwa kwenye
michuano ya klabu bingwa Afrika na Zanaco FC ya Zambia. Yanga
wameangukia kwenye michuano ya Caf Confederation Cup.
Kumekuwa na videos na picha zinazosambaa zionesha viongozi wa Azam
wakilalamika kufanyiwa fujo na mashabiki wa Mbabane kabla ya mchezo
pamoja la malalamiko ya kupulizwa kwa dawa zinazoaminika kuwa na
kemikali kwenye vyumba vya kubadilishia nguo walivyopewa Azam FC.
Mbabane wanasonga mbele kwa ushini wa jumla ya magoli 3-1 baada ya michezo miwili dhidi ya Azam FC.
No comments:
Post a Comment