Tayari Azam imeshatua Swaziland ikitokea Afrika Kusini ilikoweka kambi ya siku nne ikiwa kamili gado kwa mchezo huo huku wachezaji wa kikosi hicho wakiwa na morali kubwa ya ushindi.
Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo, mjini Mbabane, Swaziland na utaanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam, Azam FC ilishinda bao 1-0.
Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba alisema anaamini timu yake itapata matokeo mazuri katika mchezo huo, huku akiwaomba wachezaji wake kuonesha hali ya kupambana uwanjani ili kufanikisha ushindi na kusonga mbele.
Cioaba amekiri kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kwa sababu wanacheza ugenini, lakini tayari amewapa mbinu wachezaji wake ili kuwakabili vizuri wapinzani wao.
“Unapocheza ugenini unatakiwa kubadilisha baadhi ya vitu hasa kwenye mbinu, ninawaamini wachezaji wangu, ninamwamini Mungu wangu kuwa atatusaidia kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na timu yetu iweze kufuzu hatu inayofuata katika mashindano haya,” alisema Cioaba.
“Nafurahia kiwango cha timu yangu katika mchezo uliopita kwa muda mrefu timu imekuwa ikipata matokeo mazuri na inapanda hatua kwa hatua hivyo naamini hata Jumapili (leo) itapata matokeo mazuri.
Endapo Azam itafanya vizuri mchezo wa leo, itakwenda kwenye hatua ya mwisho ya mtoano, ambayo mwezi ujao itapangwa kukutana na moja ya timu 16 zilizotolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
No comments:
Post a Comment