Israel ni kati ya nchi zilizo juu katika kufanya utafiti unaohusiana na
matumizi ya bangi, huku wachambuzi wakisema kwamba hakuna hatua kubwa
iliyochukuliwa katika kukabiliana na matumizi yake.
Ingawaje kujihususha na bangi kwa namna yoyote ile unakuwa mtihani
mkubwa wa kisheria kwa maana ya kitendo batili, lakini sheria huwa
msumeno zaidi kwa wanaorudia kosa.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) inayoshugulika na dawa za
kulevya na uhalifu, takriban asilimia tisa ya raia wa Israeli ni
watumiaji wa dawa za kulevya aina ya bangi.
Hata hivyo, wataalamu hao wanabashiri kwamba, huenda kiwango hicho
kikawa juu zaidi, kwani kuna watu ambao hawakufikiwa. Huo ni kwa mujibu
wa utafiti wa mwaka 2012.
Hivi sasa kuna kamati maalumu iliyoundwa kufuatilia tatizo hilo na hasa katika bara Marekani na Ulaya.
"Kwa upande mmoja, tunajifungulia wenyewe kwa maisha ya baadaye na kwa
upande wa pili tunaelewa kwamba hata iliyopo na tunajaribu kusawazisha
mambo," anasema Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu
Katika hilo, Waziri wa Sheria, Ayelet Shaked, anatamka: "Israel haiwezi
ikafumba macho katika mabadiliko yanayofanyika duniani kuhusiana na
matumizi ya bangi na athari zake.”
Aidha, Waziri wa Usalama Gilad Erdan, anaongeza kuwa, nyendo hiyo
ilikuwa muhimu katika kutekeleza sera mpya,ya kuboresha elimu na
kupambana na uhalifu.
Sheria za Israeli zinamlenga mtu anayekamatwa kwa mara ya kwanza na
akikiri kutumia bangi, atataozwa faini ya Dola za Marekani 270 ambayo ni
sawa na Sh. 594,000.
Mtu huyo akinaswa kwa mara ya pili, faini hiyo inakuwa mara mbili ya kiwango cha kwanza, ambayo sasa inakuwa Sh. milioni 1.19.
Pia, inapokuwa kwa mara ya tatu, faini ya mara ya pili inakuwa mara
mbili ya hatua ya pili, ambayo inaongeza hadi kuwa Sh. milioni 2.376 na
inapotokea mtu anapokutwa anavuta bangi kwa mara ya nne, sasa
anakabiliwa na kesi ya jinai katika vyombo vya sheria.
Kuna wakati huko nyuma, kilinaswa kiwanda cha siri cha kuandaa bangi kwa
mfano wa sigara, ambacho kilikuwa kinaandaliwa na kuna wataalamu wa
siri wanaofanya kazi hiyo, kama ilivyo katika kiwanda cha sigara.
Ni kiwanda kilchokuwepo mafichoni katika milima iliyoko Kaskazini mwa
nchi hiyo, kilikutwa kiwanda cha siri cha kuandaa bangi na akakutwa
mtaaluma mwanamke.
No comments:
Post a Comment