Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa
masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa
sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya
kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw.
Takao Kikuchi akielezea mikakati ya KAIZEN kwa wawakilishi wa masharika
ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za
utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na
makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wawakilishi wa mashirika
ya kiserikali na makampuni binafsi wakipokea tuzo zao wakati wa sherehe
za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali
na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu toka kushoto waliokaa)
pamoja na Balozi wa Japan nchini na Mwakilishi wa JICA Tanzania wakiwa
katia picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na
makampuni binafsi walioshinda tuzo wakati wa sherehe za utoaji tuzo za
pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi
mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
Na. Eliphace Marwa – Maelezo
Watanzania watakiwa kuongeza thamani na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini.
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka watanzania kuongeza thamani ya
bidhaa na uzalishaji ili kuongeza fursa za ajira.
Mwijage ameyasema hayo wakati
akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni
binafsi wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN
zinazoratibiwa na Shirika la uhusiano wa kimataifa laJapan (JICA).
“Tuko hapa hii leo kushuhudia
sherehe za utoaji wa tuzo katika sekta ya viwanda ambayo ni matunda ya
dhana za KAIZEN kwani tuzo hizi zinatolewa kwa makampuni yaliyofanya
vizuri katika kutekeleza mbinu za KAIZEN ili kuweza kutoa changamoto kwa
makampuni mengine” alisema Mh. Mwijage
Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa
JICA ofisi ya Tanzania Bw. Toshio Nagase aliipongeza Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji pamoja na kitengo cha KAIZEN Tanzania kwa kuandaa
sherehe yenye mafanikio kwa mara nyingine kufuatia ili iliyofanyika
mwaka jana.
“Baada ya uzinduzi wa mpango wa
miaka mitano, sisi sote tumetambua umuhimu wa kukuza viwanda ili kufikia
maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa Tanzania”, alisema Bw. Toshio
Aidha Bw. Toshio alibainisha
baadhi ya maeneo ambayo KAIZEN imefanikiwa kuwa ni pamoja na kuhakikisha
ubora wa bidhaa na kubadilisha tabia pamoja na kutoa motisha kwa
wafanyakazi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi amesema kuwa anaamini kuitangaza
KAIZEN nchini Tanzania ni jambo la muhimu ili kutengeneza viwanda vyenye
ushindani na kufanikisha lengo la kukuza viwanda kuelekea mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment