Mshambuliaji Thomas Ulimwengu aliyekuwa akikipiga kwenye kikosi cha TP
Mazembe ya DR Congo, muda wowote anaweza kujiunga na Azam FC kwa ajili
ya kufanya mazoezi kabla ya kutimkia Ulaya.
Ulimwengu ambaye hivi karibuni alimaliza mkataba wake wa kuitumikia TP
Mazembe, kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam kwa mapumziko ya muda mfupi
huku mchakato wa yeye kwenda kucheza soka Ulaya ukiendelea kusukwa.
Awali ilikuwa ikielezwa kuwa, Simba na Yanga zinamtaka straika huyo,
lakini wakala wake, Jamal Kisongo, amesema kwa sasa mchezaji wake huyo
ni wa Ulaya na si kwingine kwani tayari amefanya mambo makubwa ndani ya
Afrika akiwa na TP Mazembe.
Kisono amesema kuwa: “Ulimwengu yupo Dar, kwa sasa atapumzika kwa wiki
moja bila ya kufanya mazoezi kwani ametoka kwenye majeraha, baada ya
hapo atakutana na daktari Gilbert (Kigadye) kuangalia maendeleo yake.
“Akionekana yupo fiti, ndiyo ataanza programu za mazoezi na naweza
kumpeleka Afrika Kusini au Ubelgiji kule alipo Mbwana Samatta au ajiunge
na Azam FC kwa ajili ya mazoezi.
“Huku akiendelea kulinda kiwango chake, tutakuwa kwenye mazungumzo ya
mwisho mwisho na timu tatu za Ulaya ambazo zimeonyesha nia ya
kumuhitaji, Ulimwengu si mchezaji wa kubaki tena Afrika, wala kwenda
bara lingine zaidi ya Ulaya.”
No comments:
Post a Comment