Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga
imemteuwa Jerome Dufourg kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa
miaka mitatu kuendesha klabu pamoja na kusimamia fedha.
Mfaransa huyo ambaye amewahi kufanya kazi na shirikisho la soka la
Rwanda (Ferwafa) pamoja na FC Talanta ya Kenya amepewa jukumu la
kuhakikisha klabu inapata mafanikio barani Afrika.
Lengo langu kuu itakuwa ni kutekeleza vipaumbele vya klabu ikiwemo
kuweka misingi ya kujenga soka la vijana kwa kuanzisha vituo vya kukuza
vijana wadogo, kujenga viwanja vya nyasi bandia na kutafuta mapato kwa
ajili ya hilo,” Dufourg aliimambia supersport.com alipofanyiwa mahojiano
maalum.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 anatarajia kutua Dar wiki ijayo apambapo ataanza rasmi kutekeleza majukumu yake November 19.
Mwenyekiti wa Yanga na mfanyabisha maarufu nchini Yusuf Manji anataka
kuijenga klabu ya Yanga kuwa miaongoni mwa vilabu vyenye uwezo barani
Afrika na anaamini uteuzi wa Dufourg utaisaidia Yanga kufikia malengo.
Inatajwa kuwa, mwaka uliopita mapato ya Yanga yalikuwa ni dola za
kimarekani 593,865 sawa na shilingi bilioni 1.3 za kitanzania huku
matumizi yakiwa ni dola za kimarekani milioni 1.3 ambazo ni sawa na
shilingi bilioni 2.88 za kitanzania hivyo klabu kuendeshwa kwa hasara
lakini Manji anataka Yanga iendeshwe kwa faida.
Kuhusu Mamelodi Sundowns inayoshiriki ligi ya soka ya Afrika Kusini
(PSL) kufanikiwa tutwaa ubingwa wa vilabu barani Afrika (Caf Champions
League), Dufourg amesema: “Mamelodi Sundowns wameonesha kuwa mipango na
maandalizi mazuri yanavyosaidia mataji kitu ambacho tunatakiwa
kujifunza, kujenga vilabu vyenye uwezo kama TP Mazembe ya DR Congo na
Mamelodi Sundowns.”
No comments:
Post a Comment