Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam tayari imeshatua mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC unaotarajiwa kuchezwa mwisho mwa wiki hii huku Kocha Mkuu Joseph Omog akitamba kuwa wamekuja kuchukua alama tatu muhimu.
“Tumekuja kupambana na kuondoka na alama zote kwa sababu tuna mechi mbili dhidi ya Mwadui FC na Stand United hivyo hatukuja kutalii na tunajua michezo yote itakuwa migumu kwetu ila wachezaji wangu wapo kwa ajili ya kupata ushindi”alisema Omog
Kwa sasa Simba ndio timu pekee ambayo imecheza mechi kumi na moja bila kupoteza hata mchezo mmoja na kujikusanyia alama 29 na kuwa kinara wa Ligi huku wachezaji wakiwa na morali na kiu ya kuchukua ubingwa msimu huu na wanaonekana kuwa na uchu wa mafanikio.
Ukiangalia kila idara msimu huu
imekamilika na mchezaji yoyote anayeingia anaenda kufanya kazi yake
ipasavyo na kumekuwa na wafugaji wengi pindi wanapopata nafasi ya
kutupia na kwa sasa wafungaji vinara katika timu hiyo ni Shiza Kichuya
na Mzamiru Yassin ambaye ameibuka ghafla na kuwa mwiba mkali kwa
magolikipa ambapo kila mechi anacheka na nyavu tu.
No comments:
Post a Comment