Monday, 24 October 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni
(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na
Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) aliyemtembelea na kufanya
naye mazungumzo  ,Ikulu jijini Dar es Salaam

                               
Balozi wa Italia hapa nchini Tanzania Roberto Mengoni amemhakikishia Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa nchi yake itaendelea
kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri na ya kihistoria kati ya nchi hizi
mbili katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza chachu ya maendeleo kwa
wananchi wa mataifa hayo mawili.
 
Balozi
huyo wa Italia hapa nchini ametoa kauli hiyo leo 24-Okt-2016 alipokutana
na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es
Salaam.
Balozi
huyo Roberto Mengoni ameeleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana ipasavyo
na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,utamaduni na elimu.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan ameishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kusaidia miradi ya
maendeleo ikiwemo ya afya hapa nchini.
Makamu wa
Rais amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika sekta mbalimbali
ikiwemo uimarishaji wa biashara na shughuli za utalii kati ya Italia na
Tanzania.
Amesisitiza
kuwa Serikali ipo tayari wakati wowote kupokea mawazo mazuri ya kimaendeleo
kutoka kwa Serikali ya Italia yatakayosaidia kujenga na kuimarisha ustawi mzuri
katika jamii hapa nchini.

No comments:

Post a Comment