Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam – DIT, imebuni mifumo ya TEHAMA
na kutengeneza vifaa vya kuchukulia na kupimia Mabadiliko ya Hali ya
Hewa ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji, uchakataji
na usambazaji wa taarifa hizo kwa walengwa.
Kubuniwa kwa vifaa na mifumo hiyo kutasaidia kuongeza ufanisi kwa
mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, ambayo ndiyo mlengwa namba moja wa
matumizi ya mifumo na vifaa hivyo vya kurikodi mwenendo wa hali ya hewa.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce
Ndalichako, Kesho anatarajiwa kuzindua vifaa na mifumo hiyo
itakayoambatana na warsha ya masuala ya Tehama.
Katika soko la Kimataifa, vifaa hivyo vinagharimu zaidi ya Shilingi
milion 22 lakini kwa kutengenezwa hapa nchini, vitagharimu zaidi ya
shilingi milion nne pekee.
No comments:
Post a Comment