Kocha Juma Mwambusi ndiye ataiongoza Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara
dhidi ya Ruvu JKT kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.
Mwambusi tayari amesema, hana mpango wa kuhamia Prisons na wala hajajiuzulu Yanga kama ambavyo imeelezwa.
Akili yake anaielekeza katika mechi ya leo na lengo kubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi hiyo.
Yanga inaivaa JKT ikiwa bila ya kocha wake, Hans van der Pluijm ambaye
amebwaga manyanga baada ya George Lwandamina kutoka Zambia kufika nchini
na kuzungumza na Yanga.
Aidha, Kocha wa JKT Ruvu, Malale Hamsini, ameibuka na kuwatambia
wapinzani wao Yanga kwa kusema kuwa wasifikiri watapata mteremko katika
mchezo wa leo.
Yanga leo inavaana na JKT Ruvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, ikiwa imetoka kuwachapa Kagera Sugar
mabao 6-2.
Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Malale Hamsini, amesema kuwa, siyo mara ya
kwanza kukutana na Yanga, hivyo wasifikirie watapata mteremko kutokana
na kuwafunga Kagera Sugar mabao 6.
“Kikosi chetu kipo vizuri na timu ipo kambini, hakuna majeruhi hata
mmoja zaidi ya Michael Aidani aliyekuwa majeruhi wa muda mrefu lakini
kwa sasa ameshaanza mazoezi.
“Lakini Yanga wasitegemee mteremko kwa kupata matokeo mazuri kwetu
kutokana na kuifunga Kagera Sugar mabao sita kwani tumejiandaa vizuri
kwa ajili ya mechi hiyo.
“Siyo mara yetu ya kwanza kukutana na Yanga, hivyo tunaiona ni timu ya
kawaida na kikosi chetu kipo vizuri kwa ajili ya kupambana nao,” alisema
Malale.
No comments:
Post a Comment