Na Georgina Misama-MAELEZO
Serikali imesema asilimia 90 ya
maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali wa sekta ya habari nchini
yanaohusu Muswada wa Huduma ya Habari wa mwaka 2016 yamechukuliwa na
kujumuishwa kwenye muswada huo.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi
wa Idara ya Habari MAELEZO ambaye pia ni msemaji wa serikali Bwn Hassan
Abbas wakati wa kipindi cha TUONGEE ASUBUHI kinachorushwa na kituo cha
televisheni cha Star Tv kuhusu Muswada wa Huduma ya Habari,
Bw. Abbas alisema kuwa moja kati
ya jambo la msingi ambalo serikali iliyafanya wakati wa uandaaji wa
muswada huo ni kuwakutanisha na kuwashirikisha wadau wa sekta ya habari
kutoa maoni ili kuuboresha na kwa kuzingatia umuhimu ya maoni
waliyoyatoa kwa kiasi kikubwa serikali imeyajumuisha kwenye muswada huo.
“Vitu ambavyo serikali isingeweza
kuvipuuza ni maoni ya wadau wa sekta ya habari kuhusu muswada huu na
nikuhakikishie kuwa asilimia 90 ya maoni yaliyotolewa na wadau
yamejumuishwa na lengo ni moja tu kuja na sheria nzuri itakayoiongoza
sekta ya habari na hatimaye kuiwezesha sekta hii iheshimike na iwe
rasmi” alisema Bw Abbas
Aidha, Mkurugenzi Abbas alisema
kuwa sekta ya habari ni sawa na sekta nyingine yeyote nchini, ina haki
na wajibu wake na kuwashauri wadau kuangalia zaidi upande wa haki zao
zitakazopatikana kwenye mswada huo badala ya kulalamika ili kwa pamoja
waweze kulivusha suala hili kwa ustawi wa sekta ya habari nchini.
Wakatihuo huo Bw. Abbas amewataka
wadau wa sekta ya habari nchini kuendelea kujenga hoja hasa kwenye
maeneo wanayotaka kuboreshwa kwenye muswada huu ili kuisaidia taaluma ya
habari kukua na kuheshimika kama fani nyingine nchini.
No comments:
Post a Comment