Imeelezwa kwamba watu wengi
wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kimaisha kutokana na kutokuwa na mipango
ya kimaisha ambayo wanaweza kuifanyia kazi ili waweze kufanikiwa kama
jinsi ilivyo kwa baadhi ya watu ambao wanaonekana kuwa na mafanikio.
Hayo yamesemwa na Mwandishi wa
kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka wakati wa uzinduzi wa
kitabu hcho ambacho kinnaelezea mbinu 60 ambazo zinatumiwa na watu
waliofanikiwa kimaisha kuweza kufikia alengo ambayo wamejiwekeakatika
maisha yao.
Nanauka alisema watu wengi
wamekuwa wakitamani kufanikiwa lakini wamekuwa hawajui ni hatua gani za
kupitia na kufanikiwa na baada ya yeye kufanya utafiti wa muda mrefu kwa
watu mbalimbali duniani waliofanikiwa na wasiofanikiwa, ameweza kupata
mbinu 60 ambazo ndiyo zinatofautisha watu wa matabaka hayo mawili
Alisema kupitia kitabu hicho
msmaji ataweza kufahamu ni mambo gani anatakiwa kufanya na yapi hatakiwi
kufanya ili kufanikiwa kama wengine kwa kuzingatia mbinu ambazo pia
zimekuwa zikitumiwa na watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kama
biashara, michezo, sanaa na hata uongozi.
“Watu wengi wanapenda kufanikiwa
lakini kama huna malengo huwezi kufanikiwa, watu wengi hawajui wanatumia
njia gani ili kufanikiwa na hadi wanaondoka duniani wanaondoka na ndoto
walizokuwa nazo, ndoto ambazo zilitakiwa kubaki zikifanya kazi duniani,
“Sababu ya kuandika kitabu hiki
ilianza nipotaka kujua utofauti wa waliofanikiwa na wasiofanikiwa,
aliyefanikiwa kwa aliye Marekani na Tanzania na asiefanikiwa aliye
Tanzania a Mareani, nilianza kusoa kwanini wengine wanaweza kufanikiwa
katikati ya mamilioni ya watu na baada ya kupata mawazo ya jumla ndiyo
nikapata mbinu 60 ambazo zipo katika kitabu cha TIMIZA AHADI YAKO,”
alisema Nanauka.
Nanauka alisema kitabu hicho
kitakuwa kikuzwa kwa Tsh. 10,000 na anaamini kila ambaye ataweza kusoma
kitabu hicho ataweza kupata kitu kipya ambacho kitaweza
kumsadiakufanikiwa na kufika ndoto abazo anatamani kuzifikia.
“Matumaini yangu kila atakaesoma
kitabu hiki maisha yake yabadilike kutokana na mambo ambayo atayasoma na
kila mtu hatajutia kusoma kitabu hiki, nimekiandaa kwa muda mrefu kwa
kufanya tafiti nyingi na kuweka mifano ambayo naamini itabadili maisha
ya watu wengi wataokisoma,” alisema Nanauka.
No comments:
Post a Comment