Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi,
Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakionyesha
zana walizotumia kutengeneza barabara ya Km 24 kwa nguvu zao wakati wa
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika Kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi,
Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro
wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili
katika Kijiji hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho
Gambo(Mbele kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel
Chongolo(Mbele Kulia) wakiwasili kwenye Mkutano wa hadhara katika
Kijiji cha
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha
Michael Lekule Laizer akiongea na wananchi wa Kijiji cha Esokonoi
wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Wilaya hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi
wakimskilizia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (hayupo pichani)
alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe.
Michael Lekule Laizer(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
(Katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido wakiwa katika
mavazi ya asili ya Kimasaai waliyovishwa kwa heshima na wananchi wa
Esokonoi.
Watoto wa Jamii ya Kimasaai pia walihudhuria Mkutano wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa w Arusha katika Wilaya ya Longido.
Nteghenjwa Hosseah – Longido
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Londifo, Juma Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata
na kumuweka ndani Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas baada ya
kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya zilizochangwa na wananchi wa
maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.
Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa
baada ya mara kwa mara kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila
alipokuwa akitafutwa na hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano
wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika
kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya Gilailumbwa.
Mmoja kati ya wananchi
walioshirki Mkutano huo Bi. Anni Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika
Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari
ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh Mil 96 ila
hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na
Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya
kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.
“Yaan bora umekuja Mkuu hawa
viongozi wetu huku kijijini ni Miungu watu wanajipangia mambo yao ya
kubadilisha matumizi ya Fedha zilizochangwa na wananchi kaka zao yaan
ukiwaangalia wao wana maisha mazuri wakati sisi tunateseka sasa lro
uondoke nao na tunamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hii Ndg. Mhina
kuwaleta watumishi wengine na wale waliohamishwa hapa baada ya kushirki
kula hela zetu wakamatwe pia na waseme wamepeleka wapi hela zetu”
Mara baada ya wananchi kusema
hayo Gambo alimhoji Mkurugenzi Mhina ni kwa nini hawajachukua hatua za
kisheria kuwakamata watuhumiwa ndipo Mhina aliposema mbele ya hadhara
hiyo kwamba zoezi hilo lilishindikana awali baada ya Paulo kumkwepa
Mkurugenzi huyo mara kwa mara lakini jana alijileta mwenyewe katika
mkutano huo na ndipo imekuwa rahisi kwake kumkamata.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Mkaguzi wa ndani wa Halmahauri hiyo, Bi. Mwajuma Mndaira kwenye
Mkutano huo alidai kuwa alifanya mahojiano na wenyeviti wa vijiji kujua
ni kwa nini walikusanya Fedha kwa wananchi bila kutumia stakabadhi za
Serikali katika zoezi hilo.
Pia hivi sasa bado wananendelea
na uchunguzi wa nyaraka za malalamiko mbalimbali ili kubaini Paulo
alihusika na kinanani na kwa nini abadilishe baadhi ya matumizi ya Fedha
hizo na kuuza baadhi ya vitu vilivyochangwa bila kuonyesha sababu ya
Msingi kwani baadhi ya kampuni za uwindaji wa kitalii ikiwemo Wingert
WindroseSafaris na Kampuni ya Kilombero Nothern Safaris zilitoa mifuko
ya Saruji 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari hiyo.
Rc Gambo alimuhoji Mtendaji huyo
kwanini shule hiyo haijakamilika mpaka leo wakati watoto wa jamii ya
kifugaji wana haki ya Kupata Elimu na wazazi wao wanajitoa wa ajili ya
watoto wao huku yeye akiendelea kuwarudisha nyuma, Paulo alijitetea
kwamba baadhi ya fedha hizo ziliztumika kihalali na fedha zingine
alilazimik kubadilisha matumizi yake na kujenga vyumba vya maabara, jiko
pamoja na mabweni,
Baada ya utetezi wake kugonga
mwamba alijikuta yupo chini ya himaya ya Polisi waliokuwa wakiongoza
msafara huo ambapo pia Mkuu wa Wilaya hiyo Chongolo aliahidi wananchi
hao kuwa atafuatilia suala la watumishi wengine watakoziba nafasi za
wote watakaomatwa na ubadhirifu huu kuletwa haraka iwezekanavyo ili
huduma zisizorote na endapo tuhuma hizi zikithibitkka watapelekwa
Mahakamani na aliongezwa kuwa atakua karibu nao kuhakikisha kero kama
hizo hazijitokezi rena hapo baadae .
No comments:
Post a Comment