Rais Mstaafu wa awamu ya nne
ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na washiriki wa kongamano la kuazimisha miaka 55
toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini
Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade
Aina toka nchini Nigeria akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika katika
muktadha wa Kimataifa wakati wa kongamano la kuazimisha miaka 55 toka
kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano
maalum la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka
nchini Nigeria wakati akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika katika
muktadha wa Kimataifa mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne
ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph
Sinde Warioba (kushoto) wakati wa kongamano la kuazimisha miaka 55 toka
kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema hii leo Chuoni hapo,
katikati ni Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne
ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam na Wakuu wa Vitivo wa Chuo hicho wakati wa kongamano la
kusherehekea kutimiza miaka 55 toka kuanzishwa kwa chuo hicho.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
Na: Frank Shija, MAELEZO.
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) chatakiwa kuhakikisha Chuo hicho kinaendelea kuwa kiongozi
miongoni mwa Vyuo Vikuu nchini.
Ushauri huo umetolewa na Rais
mstaafu wa awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akifungua
maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
“Hiki ndicho Chuo kiongozi kati ya
Vyuo Vikuu vyote hapa nchini, mnatakiwa kuhakikisha kinaendelea kuwa
kiongozi huku Vyuo vingine vikifuatia”. Alisema Dkt. Kikwete
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Lwekaza Mukandara amesema kuwa
pamoja na changamoto zinazo kikabili chuo hicho wanaishukuru Serikali
kwa kuendelea kusaidia katika kuleta maendeleo ya chuo hicho.
Alisema kuwa baadhi ya changamoto
zimetatuliwa kwa pamoja kati ya Serikali na wahisani ambapo alisema kuwa
ujenzi wa kumbi mpya za mihadhara, Maabara za Kisasa na jengo la
malazi,pamoja na ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea katika
Kampasi ya Julius K. Nyerere ambayo itakuwa na uwezo wa kutumiwa na
wanafunzi 4000 mara itakapo kamilika.
Akiwasilisha mada juu ya “hali ya
Taaluma Barani Afrika katika Muktadha wa Kimataifa” Mhadhiri wa Heshima
kutoka nchini Nigeria, Profesa Tade Aina amesema kuwa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam ni moja kati ya Vyuo Vikuu mahiri barani Afrika ambapo
kimetoa mchango mkubwa kwa ukombozi wa nchi nyingi za bara hili.
Aliongeza kuwa yeye binafsi ni
mnufaika mkubwa wa UDSM kwani amekuwa na ushirikiano mkubwa na baadhi ya
wahadhiri kutoka chuo hicho katika masuala mbalimbali ya taaluma.
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba
ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wakati wa uwasilishaji mada alisema kuwa
kipindi Chuo hiki kinaanzishwa aina ya masomo yaliyokuwa yanafundishwa
chuoni hapo yalikuwa na muelekeo kuandaa wafanyakazi wa Serikali kwa
wakati huo.
Na kuongeza kuwa muelekeo wa aina
ya masomo uliendelea kubadilika kadri ya siku zilivyokwenda kutokana na
mabadiliko ya teknolojia na uhitaji wa soko la ajira.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
kinaadhimisha miaka 55 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1961 kikiwa ni
tawi la Chuo Kikuu cha London, ambapo awali kilianzia katika mtaa wa
Lumumba kikiwa na wanafunzi 14 kabla ya kujengwa mahali kilipo sasa
katika eneo la Mlimani.
No comments:
Post a Comment