Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo (kushoto) akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha
Mhe. Gabriel Daqarro kwenye Kikao na wafanyabiashara wakubwa
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, lengo ni kufahamu
changamoto zinazowakabili wafanyabishara
Katibu Tawala Mkoa Mkoa wa Arusha
Ndg. Richard Kwitega(kulia) akiwa na Mkuu wa Magereza Mkoa
wakifuatilia kikao na wafanyabiashara wakubwa wa Mkoa wa Arusha
Mwenyekiti wa TATO Mkoa wa Arusha
Bw. Wilbroad Chambulu akiwasilisha malalamiko kwa niaba ya
wafanyabiashara wa Utalii Mkoa wa Arusha kwenye kikao kilichoitishwa na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Baadhi ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali walioshirki katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia(kulia) akifuatilia kikao
Mfanyabiashara Atul Nittal
(aliyesimama) na mmiliki wa Mount Meru Millers akiwasilisha malalamiko
yake katika Kikao kati ya wafanyabiashara na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mfanyabiashara Mustafa Panju
ambaye ni mmiliki wa Bush Back Safari akichangia hoja katika kuweka
mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka (AUWSA) Eng. Ruth Koya akitoa ufafanuzi wa hoja
mbalimbali zilizowasilishwa na wafanyabishara zinazohusu Taasisi yake
katika kikao hicho.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo amekutana na wafanya biashara wakubwa Mkoani
hapa na wanaolipa kodi vizuri ili kuwatambua na kuwashukuru kwa mchango
wao kwenye Uchumi wa Mkoa wa huu na Tanzania kwa ujumla. na amesisitiza
kuwa biashara zao zimechangi kwa kiwango kikubwa kuongeza ajira, na
utulivu Mkoani hapa.
Rc Gambo amewahakikishia
wafanyabiashara hao kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inawajali na iko
tayari kushirikiana nao ili kuhakikisha Changamoto mbalimbali za
kibiashara zinafanyiwa kazi na kuwatengenezea mazingira mazuri ya
kufanya biashara zao.
Aidha aliwataka Mamlaka ya
Mapato Mkoa wa Arusha kutokuwatisha wafanyabiashara na kuacha
kuwatengenezea makadirio makubwa kwani masuala kama hayo yanachochea
mazingira ya rushwa badala yake malengo hayo yaende sambamba na
uhalisia wa biashara husika .
Wafanyabiashara wakubwa wa Mkoani
Arusha wamesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais
Dkt John Magufuli umeweza kufanya vizuri sana hususani katika kufanya
kazi kwa uadilifu na kupiga vita matumizi mabaya ya fedha za umma hayo
yalisemwa na wafanyabiashara hao walipokuwa katika kikao hicho ambacho
kilifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mmoja wa wafanyabishara hao
aliyejitambulisha kwa jina la Nicholaus Duhia alisema mwaka mmoja wa
Rais Dkt Magufuli umeweza kufanya vema kusimamia ulipaji kodi, kurudisha
heshima ya uadilifu serikalini na kupiga vita ufisadi na matumuzi
mabaya ya fedha za umma zilizokuwa zikitumika kiholela bila ya kuwa na
utaratibu maalumu.
Duhia ambaye wakili, mkaguzi wa
mahesabu na ushauri wa kodi wa kampuni ya Tax Plan Associetes ya Jiji
hapa alisema kuwa hakuna anaweza kubisha kuwa hilo limefanikiwa kwa
kiasi kikubwa na kumtaka Rais kurekebisha yale yote mabaya yaliyokuwa
yakifanywa na Serikali zilizopita.
Alisema na kutoa ombi kupitia kwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuwa Rais Dkt Magufuli katika mwaka wa pili wa
uongozi wake anapaswa kurudisha imani kwa wafanyabiashara wa hapa nchini
ili waweze kufanya kazi bila ya woga.
Naye Sailesh Pandit Mkurugenzi
Mtendaji wa A lodhia Group Enterprises alisema kuwa mbali ya kumkubali
Rais Dkt Magufuli kwa utendaji kazi wake wa hapa kazi tu alisema kuwa
heshima ya kazi serikali imeimarika na watendaji wa serikali wanachapa
kazi haswa haswa.
Pandit alisema kuna kasoro chache
ambazo zinapaswa kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na yeye kuzuiliwa
kusambaza bomba za plastic na kusema kuwa kazi hiyo inafanywa na viwanda
vya Jijini Dar es salaam tu.
Alisema na kumtaka Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo kuingilia hilo kwani kwa kufanya hivyo kutafanya
viwanda vingi Mkoani Arusha kufungwa na azma ya Rais ya uchumi wa
viwanda haitakuwa na maana yoyote.
Mkurugenzi huyo wa Lodhia alisema
kiwanda chake kiko kwa zaidi ya miaka sita na kimeingia katika
ushindani wa zabuni wa kusambaza bomba katika Mamlaka za maji hapa
Arusha lakini kazi hizo zimekuwa zikipewa kampuniza Jijini Dar es salaam
hali inayowafanya kukata tama.
‘’Kiwanda changu cha Plastic
Arusha kimepigwa vita kisifanye kazi ya kusambaza bomba na kuteuliwa
viwanda vya Dar es salaam hii ni mbaya sana mkuu wa mkoa ‘’ alisema
Pandit
Alisema kiwanda hicho
kimekaguliwa na Mamlaka zote za serikali kwa zaidi ya miaka sita
iliyopita lakini baadhi ya taasisi zingine zinaweka ugumu bila ya sababu
za msingi kwa kiwanda hicho kutopewa kazi.
Wafanyabiashara wengine Willbroad
Chambulu wa Kibo Safari na Atul Nittal wa Mount Meru Millers wamesema
kuwa serikali ya awamu ya tano iangalia namna ya kupunguza utitiri wa
kodi kwa wafanyabiasha wakubwa.
Wakati huo huo Mfanyabiashara
Willbroad Chambulu alikabidhi majina ya kampuni za Utalii zaidi ya 500
ambazo hazipo kwenye orodha ya Mamlaka ya Mapato Mkoani ili ziweze
kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa mapato.
Gambo aliwahakikishiwa
wafanyabiashara hao kuwa Serikali yao itakuwa imara na ipo tayari
kuwasaidia pale watakapo kwama, lengo ni kutaka wafanye kazi kwa ufanisi
bila ya kipingamizi.
No comments:
Post a Comment