Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli leo Oktoba 29, 2016 anasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
ambapo anatimiza miaka 57.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa ‘twitter’ Rais Dkt.
Magufuli amewashukuru watanzania wote kwa kumtakia heri na kuahidi
kuendelea kuchapa kazi kwa maslahi ya taifa.“Ninamshukuru Mungu kufikia siku yangu ya kuzaliwa,ninawashukuru watanzania nyote kwa kuniombea , nitafanya kazi kwa moyo na nguvu zangu zote” Amesema Rais Dkt. Magufuli.
Aidha Rais Dkt. Magufuli anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ikiwa anakaribia kutimiza mwaka mmoja tangu alipoapa kuliongoza taifa la Tanzania Novemba 5, 2015.
Rais Dkt. Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 katika Wilaya ya Chato ambayo ni mojawapo ya wilaya tano za mkoa mpya wa Geita uliopo kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Wilaya ya Chato ilikuwa sehemu ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera na ni mwaka 2012 tu ndipo ilipohamishiwa Mkoa wa Geita.
No comments:
Post a Comment