Mkuu wa mkoa wa Pwani
mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza baraza la wafanyakazi mkoani humo
katika kipindi cha mwaka 2016/2019(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mkuu wa mkoa wa Pwani
mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka maafisa utumishi kuwapa nafasi
baadhi ya wafanyakazi wanaoomba kwenda kujiendeleza kitaaluma badala ya
kuwabania na kusababisha kudumaa kielimu.
Aidha ametoa rai kwa
watumishi wa umma mkoani humo kuwajibika kwenye maeneo yao ya kazi
pamoja na kuwatumikia wananchi kikamilifu.
Mbali na hayo mkuu huyo
wa mkoa ,amesisitiza viongozi mbalimbali kwenye maeneo ya kazi kujenga
ushirikiano wa kutosha na watumishi ili kuondoa malalamiko ambayo huwa
yakijitokeza .
Mhandisi Ndikilo
aliyasema hayo ,wakati akifungua baraza la wafanyakazi mkoani Pwani
mwaka 2016-2019 pamoja na kuchagua katibu na katibu msaidizi wa baraza
hilo.
Hata hivyo alisema ni
lazima kukubaliana na mabadiliko na kwenda na wakati kwa kukuza taaluma
za watumishi ili kuongeza uwezo kwenye maeneo yao ya kazi .
“Kiukweli tuliyojifunza
darasani isiwe mwisho badala yake tuongeze elimu zetu kwa lengo la
kupanua elimu zetu ambazo wengi wetu tumezipata miaka mingi iliyopita”
alisema.
Mhandisi Ndikilo,
alieleza kuwa ifikie wakati wa kujitambua na kuthamini nafasi walizonazo
na kutamani kufika kwenye hatua nzuri ya kielimu.
Akizungumzia suala la
uwajibikaji aliwaomba maafisa utumishi na makatibu tawala wilaya na
mkoa waendelee kuwa wawakilishi wakubwa wa kuwasilisha kero
zinazowakabili watumishi .
Alisema uwajibikaji kazini ni nguzo pekee ya ufanisi kazi hivyo kuna kila sababu ya viongozi kuwa na ushirikiano na watumishi .
“Wote tupo sawa na
kila mmoja anafanyakazi kwenye nafasi yake ,hakuna mkubwa zidi ya
mwenzie kwa kumfanya mwengine amsujudie hadi kuogopana kazini.
” Kikubwa ni
kuheshimiana ,kuwa na upendo na kuthaminiana bila kudharauliana ama
kutokana na nafasi yako ya juu ndio ukandamize wengine.alisisitiza.
Nae afisa kutoka ofisi
ya waziri mkuu ,kazi,ajira,vijana na wenye ulemavu ,Honesta Ngolly
aliyataka mabaraza ya wafanyakazi yatumie meno yake kusimamia kero za
wafanyakazi.
Alisema watumishi wana haki ya kujiendeleza kielimu na hakuna serikali ambayo imekataza watumishi kujiendeleza.
Honesta alisema endapo watumishi watakuwa wakiongeza elimu zao itawezesha kuongeza ufanisi makazini.
Mwenyekiti wa baraza
la wafanyakazi mkoani Pwani Edward Mwakipesile alisema mawazo na
maagizo waliyopewa watayafanyia kazi ili kulinda maslahi na haki za
watumishi.
Mwakipesile aliomba
ushirikiano na uwajibikaji uendelee katika mkoa huo ili kupiga hatua
kutoka mkoa ulipo na kuwatumikia wananchi .
Awali kabla ya
kufunguliwa baraza hilo Pascal Dawson alichaguliwa kuwa katibu wa
baraza la wafanyakazi mkoani hapo na katibu msaidizi Asha Itelewe.
No comments:
Post a Comment