Mbunge
wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa vijiji
vya Mbunju na Mbambe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuwatembelea kwa
ajili ya kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza
kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
Baadhi ya wakinamama wajawazito wanaoishi katika vijiji vya Mbunju na Mbambe vilivyopo kata ya Mkongo
Wilayani
Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya muda mrefu
ya kujifungulia wakiwa njiani kutokana na kuwepo kwa umbali mrefu
kutoka makazi wanayoishi hadi kufika katika zahanati au kituo cha afya
kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wakinamama
hao wametoa kilio chao wakati walipotembelewa na mbunge wa jimbo la
Rufiji ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza
kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wake pamoja
na kero zao ili kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuleta
chachu ya maendeleo.
Zarau
Kiambwe Tabia Athumani,pamoja na Suzan Masela ni miongoni mwa
wakinamama hao wanaokabiliwa na changamoto hiyo,walisema wakati
mwingine wanapata wakati mgumu hususan nyakati za usiku kutokana na
kukosa usafiri hivyo kuwalazimu kujifungulia njiani hali ambayo
inahatarisha uhai wa kupopteza maisha yao ukizingatia na gharama za
usafiri wa piki piki ni kubwa hivyo wanashindwa kuzimudu kutoka na
kutokuwa na kipato chochote.
Aidha
wakinamama hao wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo la Rufiji kwa
kushirikianana serikali ya awamu ya tano kuliingilia kati suala hilo ili
kuweza kuwasaidia wananchi kwa kuwajengeaa zahanati pamoja na vituo
vya afya vilivyvyo karibu na maeneo wanayoishi ili kuweza kupata huduma
ya matibatu kwa urahisi bila ya usumbufu.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa baada ya
kusikiliza kilio cha siku nyingi kutoka kwa wakinamama hao amesema
kwamba atahakikisha anashirikina bega kwa bga na viongozi wa halmashari
pamoja na serikali katika kujenga zahanati na vituo vya afya sambamba
na kuongeza idadi ya wauguzi pamoja na madaktari.
Mchengrwa
alisema kwamba katika kuunga juhudi za serikali katika kuboresha
sekta ya afya atahakikisha anaweka mipango madhubuti kwa kuongeza idadi
ya ujenzi wa majengo ya huduma za afya ili kuweza kuwafikia kwa urahisi
wananchi katika upatikanaji wa matibabu bila ya kusafiri kutembea
umbali mrefu.
“Dhamira
kubwa ya serikali hii ya awamu ya tano ni kuhakikihs huduma ya afya
inakuwa karibu na jamii ambayo inatuzunguka, hivyo kwa upande wangu kama
Mbunge wa Jimbo hili la Rufiji nitakuwa mstari wa mbele katika
kushirikina na viongozi wa halmashauri lengo ikiwa ni kuwaondolea kero
wananchi ya kufuata huduma mbali, hivyo katika hili nitalisimamia kwa
hali na mali,”alima Mchengerwa.
Changamoto
ya baadhi ya wakinamama katika maeneo mbali mbali ya Wilani Rufiji
Mkoani Pwani ya kujifungulia wakiwa njiani bado inaonekana bado kuwa ni
tatizo sugu na hii ni kutokana na kuwepo kwa umbari mrefu wa kuzikia
zahanati pamoja na vituo vya afya hivyo kusababisha kero na usumbufu
mkubwa pindi mgonjwa anapohitajika kupelekwa kwa ajili ya kupatiwa
matibabu hivyo ni jukumu la serikali kuboresha sekta ya afya katika
kukabiliana na hali hiyo.
No comments:
Post a Comment