Kongamano kuhusu mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia litafanyika Jumamosi Oktoba 22 mwaka huu ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na litarushwa live (mubashara) na kituo cha televisheni cha Azam.
Kongamano
hilo limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA), likiwa na lengo la kupata maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo
hiyo, ambapo Simba ipo mbioni kuingia mambo ya hisa, wakati Yanga
utaratibu wa kukodishwa.
Kongamano
halina nia ya kuzuia mabadiliko au kuharakisha mabadiliko katika klabu
hizo, badala yake inataka litumike kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wa
mpira wa miguu kuhusu mifumo hiyo na aina nyingine ya mifumo ya
uendeshaji wa klabu duniani, hivyo kusaidia kujibu maswali mbalimbali ambayo pengine hayajibiwi ipasavyo.
Baadhi
ya mambo yatakayozungumziwa ni umuhimu wa mabadiliko katika klabu hizo,
pia harakati za kuzibadili zilivyoanza miaka ya nyuma na matokeo yake
na itazungumziwa pia mifumo ya uendeshaji ya klabu mbalimbali duniani.
Lengo
ni kujadili kitaalamu bila ushabiki wa namna yoyote kwani nia ni
kujenga na kuimarisha soka na michezo kwa ujumla hapa nchini na ndiyo
sababu tumealika wataalamu wa kada mbalimbali, viongozi wa zamani wa
soka kwa tofauti na baadhi ya wadau wa soka.
Tunaomba
mashabiki na wadau wengine mbao hawakualikwa watambue tunathamini
mawazo yao, lakini nafasi ya wanaotakiwa kuhudhuria ni chache hivyo
wafuatilie kupitia vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment