Miongoni mwa wadau walioalikwa na kamati kutoa maoni yao ni pamoja na baraza la habari Tanzania, jukwaa la wahariri, shirikisho la waandishi wa habari UTPC umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari na chama cha wanasheria Tanganyika.
Wadau kwa pamoja wamegomea kutoa maoni yao wakidai muda wa mushwada huo utakaowasilishwa na kujadiliwa kwenye bunge lijalo na kisha kutungiwa sheria ni mdogo ukilinganishwa na ukubwa wa tasinia na umuhimu wake hatua iliyomlazimu mwenyekiti wa kamati kuwapa juma moja kujadili lakini hata hivyo wamedai hawako tayari.
Kwa upande wake waziri kivuli wa wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo Mhe Joseph Mbilinyi Sugu ameitaka serikali kukaa meza moja na wadau ili kujadili muswada huo na kufikia muafaka kwani kama hautakuwa na maridhiano huenda ukaondoa uhuru wa wananchi kupata habari ambao unatambulika kikatiba.
Nje ya ukumbi wa kamati wadau wa habari wanakutana na wanahabari na kisha kueleza ni nini hasa kilichowapelekea kugomea kutoa maoni huku wakidai muswada huo unamapungufu kadhaa na unahitajika kwanza uwafikie wanahabara wote kwa ajili ya kutoa maoni yao na kisha ndio upelekwe bungeni.
No comments:
Post a Comment