Dkt.Kigwangwalla akizinduz moja
ya kitabu cha Mkakati wa kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa
ulizinduliwa jana mkoani Dodoma na kugawiwa kwa waganga wakuu wote
nchini,kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt.Zainabu
Chaula,kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed Bakari Kambi
Dkt.Kigwangwalla akionesha moja
ya kitabu hicho kilizhozinduliwa leo na kugawiwa kwa waganga wakuu wote
nchini,kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt.Zainabu
Chaula,kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed Bakari Kambi
Naibu Waziri wa Afya akimkabidhi mkakati huo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Profesa Maseru.
Naibu Waziri wa Afya akimkabidhi mkakati huo Naibu katibu Mkuu Tamisemi Dkt.Zainabu Chaula
Dkt.Kigwangwalla akimkabidhi mkakati wa Taifa wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed Bakari Kambi
ibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwalla akiwahutubia
waganga wakuu wa mikoa na wilaya wakati wa uzinduzi wa mkakati wa Taifa
wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwenye mkutano wa mwaka wa wakuu hao
unaoendelea mjini Dodoma
HOTUBA YA NAIBU WAZIRI MH. DK. KIGWANGWAALLA
Napenda kumshukuru Mwenyezi
Mungu aliyetuwezesha kukusanyika hapa siku ya leo. Pia, ninayo furaha
kubwa kusimama mbele yenu kama mgeni rasmi katika kuzindua mkakati huu
muhimu wa pili wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Pamoja na
rasilimali chache tulizonazo, Tanzania imepiga hatua kidogo katika
kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi
sana duniani na haswa nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwemo. Utafiti
uliofanyika na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Afya duniani na Taasisi ya NIMR,
ya viashiria vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza imeonyesha kuongezeka kwa
viashiria hivyo. Idadi ya watu wanaovuta sigara ni asilimia 15.9%,
wanaokunywa pombe ni asilimia 29.3%, wenye uzito uliopita kiasi 34.7%,
shinikizo la damu ni asilimia 25.9% na wagonjwa wa kisukari ni asilimia
9.1%. Hii haikubaliki, na ni lazima tuongeze bidii katika
kuyashughulikia.Mkakati huu umekuja wakati muafaka, wakati tunatakiwa kutekeleza Mpango wa Malengo endelevu (Sustainable Development Goals) ambayo kati ya malengo kumi na saba, matatu yanazungumzia jinsi ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, baadhi ya malengo haya ni;
Kufikia mwaka 2030, kupunguza moja ya tatu ya vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kukinga, kutibu na kuzingatia afya ya akili;
Kuboresha huduma za kinga na tiba ya utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe;
Kufikia mwaka 2020, kupunguza nusu ya idadi ya vifo duniani na ajali za barabarani.
Napenda kutambua mchango mkubwa uliotolewa na Chama cha kupambana na ugonjwa wa kisukari duniani (World Diabetes Foundation) na chama cha kisukari cha Tanzania (Tanzania Diabetes Association), kwa kuwezesha kupitiwa kwa mkakati wa zamani wa mwaka 2008-2015, na kutengenezwa huu wa sasa, ambao ni wa 2016-2020. Kwa kushirikiana na kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, TDA imeweza kutekeleza mpango wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchi nzima.
Aidha nawashukuru kwa dhati wadau wetu wa Maendeleo kwa misaada mbalimbali ambayo imechangia katika kuboresha Afya za Watanzania.
Ninayo taarifa kuwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya mmeombwa kuteua mtu mmoja atakayeratibu shughuli zote za magonjwa yasiyo ya kuambukiza mikoani na wilayani kwenu. Ni matarajio yangu kuwa mtafanya kazi kwa nguvu na kwa ukaribu zaidi na kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza cha Wizara ili huduma hizi ziwafikie watu wote hadi ngazi ya jamii.
Baada ya kusema haya machache , sasa natamka kuwa Mkakati huu wa pili wa kitaifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza umezinduliwa rasmi.
No comments:
Post a Comment